Watu
wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti yaliyotokea
mkoani Singida mwishoni mwa wiki likiwemo la mfanyabiashara kujipiga
risasi kichwani na mwingine huchinjwa shingo, kutolewa koromeo na ulimi.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
Geofrey Kamwela alisema katika tukio la kwanza, mfanyabiashara Mashaka
Omari (30) alikutwa chumbani kwake Mtaa wa Ipembe akiwa amekufa baada ya
kujipiga risasi kichwani. Alisema mfanyabiashara huyo alijiua kwa
kutumia bastola yake yenye namba TZ CA 895101 ambapo polisi walikuta
ganda moja la risasi iliyotumika lakini magazini ilikuwa na risasi 11,"
alisema Kamanda Kamwela. Uchunguzi...
Padri anayedaiwa kutelekeza mtoto kuburuzwa kortini tena leo
Mahakama
ya Mwanzo Utemini iliyopi mjini hapa Mkoa wa Singida, leo inatarajia
kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili Padri wa Kanisa Katoliki mjini
hapa, Deogratius Makuri ya kumtelekeza bila kumhudumia mtoto wake wa
kike aliyedaiwa kuzaa na muumini wake.
Kesi hiyo ilisikilizwa wiki iliyopita na kuahirishwa baada ya kudaiwa
mahakamani hapo kuwa padri huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda
mrefu na Maria Boniphance (26) aliyekuwa mhudumu wa kanisa hilo Parokia
ya Singida mjini.
Ilidaiwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ferdnand Njau kuwa wakati
wote huo wa mahusiano ya kimapenzi, ndipo mshitakiwa alimpa ujauzito na
kuzaa naye mtoto wa kike.
Mlalamikaji (Maria) alidai mahakamani hapo kuwa baada ya ujauzito huo,
aliamua kulifikisha...
Ikungi kutumia bil. 25/-
HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, inatarajia kutumia
shilingi bilioni 25.696 katika mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya
matumizi ya kawaida na shughuli za maendeleo.
Akisoma taarifa ya bajeti kwenye kikao maalumu cha Baraza la Madiwani
wa halmashauri hiyo jana, Makamu Mwenyekiti Ally Nkangaa, alisema
katika kipindi hicho kiasi cha sh bilioni 15.426 ni kwa ajili ya
mishahara ya watumishi wake.
Hata hivyo alisema katika bajeti iliyopita halmashauri iliomba
kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 16.953 ambapo hadi kufikia mwezi
Desemba mwaka huu, jumla ya shilingi milioni 512.322 zilikuwa
zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Nkhangaa alisema katika utekelezaji wa bajeti, zipo changamoto
mbalimbali ambazo...
Mvua kubwa zaleta madhara Singida, watu watano wahofiwa kufa maji
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tukio la maafa ya
mvua kubwa iliyosababisha vifo.
Na Nathaniel Limu, Singida
MVUA
kubwa zilizoanza kunyesha mkoani Singida zimeanza kuleta maafa baada ya
watu watano kuhofiwa kufa maji kutokana na gari waliolokuwa wakisafiria
kusombwa na maji ya mto.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo limetokea Desemba saba mwaka huu saa 3:30 asubuhi huko katika mto
wa Nzalala kijiji cha Kisimba tarafa ya Kisiriri wilayani Iramba.
Amesema
siku ya tukio, abiria...
MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA MKOANI SINGIDA.

TUNAOMBA RADHI KWA HII PICHA
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,akionyesha bunduki ya
kijeshi aina ya SMG no.34555 iliyokuwa ikitumiwa na watu wawili
wanaodhaniwa kuwa majamabazi katika kijiji cha Manga manispaa ya
Singida.
WATU
wawili wakazi wa manispaa ya Singida ambao majina yao bado
hayajajulikana,wakiwa kwenye Jokofu la kuhifadhia maiti baada ya kuuawa
wakati wa majibishano ya risasi na polisi.
JESHI la Polisi mkoani Singida limewauwa watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP, Geofrey Kamwela...
WATANO WAFA MAJI NA WENGINE 11 WANUSURIKA
WATU
watano wanahofiwa kufa maji na wengine 11 wamenusurika, baada ya gari
waliyokuwa wakisafiria kusombwa na maji ya mto kufuatia mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha mkoani mkoani Singida.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Kamishina msaidizi
mwandamizi Geofrey Kamwela, tukio hilo limetokea jana majira ya saa
3: 30 asubuhi katika Kijiji cha Kisimba Wilayani Iramba.
Amesema watu hao waliokuwa wakisafiri kwa gari yenye namba za usajili
T.499 ATR aina ya Land rover 110 TDI, walikuwa wakijaribu kuvuka mto
Nzalala kutoka eneo Doromoni kwenda Kiomboi Mjini.
Kamanda
Kamwela amesema wakati dereva ambaye hajatambuliwa jina wala makazi
akijaribu kuvusha, gari hiyo ilizimika katikati ya mto kabla ya
kosombwa na maji ikiwa na abiria 16 ndani.
Amesema
...
Ajali yaua watano
Singida.Abiria watano wamekufa baada ya gari
aina ya Landrover 110 waliyokuwa wanasafiria kusombwa na maji katika
Kijiji cha Doromoni Wilaya ya Iramba.
Katika ajali hiyo iliyotolea jana, watu wengine 11 walinusurika baada ya kuruka na kuogelea mara baada ya gari hiyo kupinduka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Kamwela alisema ajali hiyo ilitokea majira ya
asubuhi wakati gari hilo likiwa linabeba abiria 16 kutoka Kijiji cha
Doromoni wilayani Iramba kuelekea Kiomboi mjini.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni kujaa kwa maji katika Mto Nzalala kiasi cha kulifunika daraja.
...
Polisi yaua majambazi wawili
JESHI la Polisi mkoani Singida limewaua kwa kuwapiga risasi
majambazi wawili waliokuwa wakijiandaa kufanya uhalifu katika Kijiji cha
Manga nje kidogo ya mji wa Singida.
Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Godfrey Kamwela alisema tukio hilo
limetokea juzi, saa 12:00 jioni baada ya polisi kupata taarifa za siri
kutoka kwa raia wema.
Kamwela alisema majambazi hayo yalikuwa na bunduki moja aina ya SMG
yenye namba 34555 ikiwa na risasi saba kwenye magazine, huku wakitumia
pikipiki T 634 BTW Sanlg.
Aidha, Kamanda Kamwela alisema askari polisi walifika katika eneo
hilo, na watu hao walistuka kwa kuwa wanafuatiliwa na askari na hivyo
kuanza kukimbia kuelekea Kijiji cha Uhamaka kwa kutumia pikipiki hiyo.
Hata hivyo,...
Ofisi ya mtendaji Kondoa yafungwa
OFISI ya mtendaji wa kijiji cha Salanka, kata ya Salanka, wilayani
Kondoa, imefungwa kwa kukosa mtendaji wa kijiji kwa muda wa mwaka moja
sasa.
Hali hiyo imeelezwa kuchangia wananchi kukosa huduma hivyo na
kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo kwenye ofisi ya
kata.
Mtendaji wa kijiji hicho alisimamishwa na mkutano wa kijiji kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kijiji.
Akizungumza kwenye mkutano wa kijiji, Mwenyekiti wa kijiji hicho,
Khamis Majaliwa, alisema wamekuwa wakifuatilia suala hilo kwa muda sasa
huku Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Ndani wa halmashauri hiyo akifika
mara moja na hadi sasa hajafika kijijini hapo kwa madai ya kukosa
usafiri.
Katika mkutano huo, wanakijiji hao waliazimia kwenda kuonana na Waziri
Mkuu kutatua tatizo hilo...
MSIMAMO WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA DHIDI YA MAAMUZI YA KAMATI KUU - TAARIFA KWA UMMA

WILFRED NOEL KITUNDU
MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza...
Wajasiriamali waelezwa umuhimu wa soko la hisa
MKUU
wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, ameelezea umuhimu wa soko la hisa
katika upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu na uwekezaji kuwa haviwezi
kuletwa na masoko ya mitaji pekee.
Kwa mujibu wa mkuu huyo, dhima ya kupata rasilimali na kuzitumia
kikamilifu kwenye miradi yenye tija, husababisha ukuaji wa uchumi na
kuongeza utajiri.
Dk. Kone amebainisha hayo juzi mjini Singida wakati akifungua semina
ya siku mbili kwa wafanyabiashara na wajasiriamali juu ya soko la kukuza
ujasiriamali (EGM) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Aque Vitae.
Alisema ni muhimu ieleweke wazi kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja
baina ya mafanikio ya...