Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KIKOSI
cha Kuzuia Ujangili (KDU) Kanda ya Kati, kimefanikiwa kukamata
majangili 692 na meno ya tembo 195 katika Operesheni Tokomeza Ujangili
iliyofanyika wilayani Manyoni, Singida kuanzia mwaka 2009 hadi 2012.
Kaimu Meneja wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rungwa, Batholomeo
Mganga, alisema hayo wakati wa kumkabidhi baiskeli ya miguu mitatu
mlemavu, Yohana Pangarasi, mwanakijiji wa Imalampaka, Manyoni.
Mganga alisema katika kipindi hicho tembo 168 wenye uzito wa kilo 166 waliuawa na majangili hao kinyume cha sheria.
Hata hivyo Kaimu Meneja wa KDU alisema mwaka 2009 licha ya kukamatwa
kwa majangili 116, tembo 16 waliuawa wakati mwaka 2010 majangili 172
walikamatwa wakiwa na meno ya tembo manne yaliyokuwa na uzito wa kilo
23.5
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment