Kaimu
meya mstahiki wa manispaa ya Singida, Hassan Mkata akizungumza kwenye
kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Singida
kilichofanyika mkoani Singida.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya
Singida. Robert Mahili na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM manispaa ya
Singida,Hamisi Nguli.
Diwani
wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku, akichangia hoja katika kikao cha
baraza la madiwani wa manispaa ya Singida kilichofanyika mjini Singida.
Afisa
Ardhi manispaa ya Singida, Angelus John Camara,akitoa ufafanuzi juu
ya sheria ya Ardhi mbele ya kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika
mkoani Singida.
Baadhi
ya madiwani wa manispaa ya Singida waliohudhuria kikao cha kawaida cha
baraza la madiwani kilichofanyika mjini Singida.(Picha na Nathaniel
limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
KUTOKANA
na uhaba mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya katika vituo mbalimbali
vya afya vikiwemo zahanati,serikali imeshauriwa kuajiri waganga wa jadi
ili kupunguza uhaba huo.
Ushauri
huo wa bure,umetolewa hivi karibuni na Diwani wa kata ya Unyambwa (CCM)
Manispaa ya Singida,Shaban Satu wakati akichangia hoja ya diwani wa
kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku ambaye alidai zahanati ya kata yake
imekuwa na mhudumu moja tu kwa kipindi kirefu.
Amesema uzoefu unaonyesha kuwa uhaba wa wahudumu wa afya una athari nyingi ikiwemo ya utoaji wa huduma usiokidhi mahitaji.
“Diwani
mwenzetu ametueleza kwamba kwa muda mrefu amefikisha tatizo la uhaba wa
wahudumu katika ngazi husika mara nyingi,lakini juhudi zake hazijazaqa
matunda hadi sasa”,amesema.
Amesema
endapo serikali imeshindwa kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo
hilo,basi ni bora ikatoa nafasi kwa waganga wa jadi kuziba mapungufu
hayo”,alifafanua.
Katika hatua nyingine,imedaiwa kuwa shule ya msingi ya kijiji cha Mwankoko,inakabiliwa na uhaba wa madawati 316.
Kaimu
Mkurugenzi wa manispaa hiyo,Robert Mahili aliiomba serikali ya kijiji
hicho kuongeza juhudi zaidi kuhamasisha wananchi kuchangia ununuzi wa
madawati.
Amesema
pia juhudi zilifanyika za za kuzishawishi benki ya NBC,CRDB,NMB na
CIP,ili ziweze kusaidia kuondoa uhaba huo mkubwa wa madawati.
Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi,Mahili,manispaa hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu 298.
0 comments:
Post a Comment