ABIRIA waliokuwa wanasafiri kutoka Dodoma kuelekea mikoa ya kanda ziwa, magharibi na nchi jirani, leo asubuhi wamekwama kwa zaidi ya saa nne katika eneo la Kijiji cha Kisaki umbali wa Kilomita 10 kabla ya kufika Singida mjini baada ya madereva wa malori kufunga barabara .
Zaidi ya malori 300 yaliegeshwa barabarani kuanzia saa 12 hadi saa 4 asubuhi, kuzuia magari mengine yasipite ili kulishinikiza jeshi la polisi kudhibiti uhalifu wa mara kwa mara katika eneo hilo baada ya wenzao wawili kutekwa na majambazi, kujeruhiwa kisha kuporwa fedha na mali nyingine.
Madereva hao wamesema wamefikia uamuzi wa kufunga barabara ili kuwasilisha hisia zao kwa mamlaka husika baada ya eneo hilo na utekaji magari mara.
Wamesema mbali na kuporwa fedha na mali nyingine, pia wamekuwa akijeruhiwa kwa mapanga, pinde na silaha za moto kiasi cha kuhatarisha maisha yao lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.
Madereva hao wamekubali kuendelea na safari baada ya Naibu Waziri wa Ushiriano wa Afrika Mashariki Abdulla Juma Abdull aliyekuwa miongoni mwa watu walikwama eneo hilo, kuahidi kuifikisha kero hiyo kwa mamlaka husika na ufumbufu wa kudumu kutafutwa haraka iwezekanavyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida Geofrey Kamwela amesema polisi wanaendelea na msako mkali dhidi ya watu waliofanya utekaji huo wa magari na kupora madereva fedha pamoja na kuwajeruhi.
Hata hivyo ametoa wito kwa wadau wote kushirikiana kudhibiti uhalifu badala ya kufunga barabara na kuwategemea polisi peeke ambao ni wachache na hawawezi kuwepo kila mahali penye uhalifu.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment