Kamanda
 wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na
 waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
WAFANYABIASHARA
 wa Manyoni mjini mume na mke,wametekwa na watu watatu waliojifanya kuwa
 ni maafisa usalama wa taifa makao makuu jijini Dar-es-salaam.
Waathirika wa utekaji huo ni Methew Dominik @ Cheupe (46) na mke wake Selina Methew (42).
Kamanda
 wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio 
hilo limetokea juzi saa tisa alasiri Manyoni mjini.
Amesema
 Faraja George (35) mfanyabiashara wa Dodoma mjini,mganga wa tiba asilia
 na mkazi wa mkoa wa Tanga,Saidi Mgolola @Pesa mbili (49) Michael Peter 
 na Michael Peter (26) mkazi wa Moshi mjini na dereva wa gari 
lililotumika katika utekaji huo.
Amesema
 siku ya tukio watuhumiwa wakiwa na gari T.242 CBM aina ya toyota 
prado,walifika dukani kwa Methew baada ya kudai kuwa wao ni maafisa 
usalama taifa,walimwamuru mwenye duka kuwa wanamhitaji Singida mjini kwa
 ajili ya mahojiano.
“Methew
 aliwaomba maafisa hao bandia kuwa aambatane na mke wake huko kwenye 
mahojiano hayo.Baada ya waathirika hao kuingia ndani ya gari,gari hilo 
badala ya kuelekea Singida mjini,lilibadili na kuelekea Dodoma”,amesema.
Kamwela
 amesema bahati nzuri polisi Manyoni mjini walipata taarifa ya tukio 
hilo mapema na wakawasiliana na wenzao wa Bahi mkoani Dodoma ambao 
walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa hapo kwenye kizuizi.
Amesema
 uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo,ni watuhumiwa 
kutaka kumwibia mali mfanyabiashara hiyo Methew.Uchunguzi zaidi bado 
unaendelea.
Kamwela amesema kuwa mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
Mo Blog 
0 comments:
Post a Comment