Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI
la Polisi mkoa wa Singida linamshikilia Mariamu Songeraeli (32) mkulima
mkazi wa kijiji cha Nselembwe wilaya ya Iramba kwa tuhuma ya kumiliki
madawa ya kulevya aina ya bhangi misokoto 88 yenye uzito wa gramu 44.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema
mtuhumiwa Mariamu amekamatwa juzi saa 11.30 jioni nyumbani kwake katika
kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui wilaya ya Iramba.
Amesema
askari polisi waliokuwa kwenye doria siku ya tukio,walipata taarifa
kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa Mariamu anajihusisha na biashara
haramu ya kununua na kuuza bhangi.
Kamwela
amesema askari hao waliweza kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa na kuipekua
na kisha kuikuta misokoto hiyo ya bhangi ikiwa chumbani kwake,imefichwa
kwenye mfuko wa rambo.
“Tunamshikilia
mtuhumiwa kwa uchunguzi zaidi,ili kujua ni wapi anakoitoa bhangi hiyo
na watu anaoshirikiana nao katika bishara hiyo haramu,baada ya uchunguzi
huo kukamilika,atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
inayomkabili”,amesema.
Aidha,Kamwela
ametumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza raia wema kwa kutoa
taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu,na kuwaomba waendelee na moyo huo
huo,kwa madai kwamba suala la usalama ni la wananchi wote kwa ujumla.
Chanzo Mo Blog
0 comments:
Post a Comment