Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela (pichani), 
alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 1:30 asubuhi katika kijiji 
cha Nkalankala tarafa ya Nduguti, wilaya Mkalama.
Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni bibi wa mtoto huyo, Neema Paulo (35) na mama wa marehemu, Hidaya Omari (20).
Alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kabla ya kufikwa na mauti,
 mtoto huyo alinyongwa shingoni, kuchunwa ngozi sehemu zake za siri na 
wauaji kutoweka nazo, kisha mwili wake kutumbukizwa ndani ya kisima 
kilichokuwa na maji.
Kamwela alisema kuwa mwili wa mtoto huyo baadaye ulionekana baada ya kuelea juu ya maji na wananchi kutoa taarifa polisi.
"Mauaji haya yanahusishwa na imani ya kishirikina kutokana na 
kuchunwa ngozi na kunyofolewa sehemu za siri...lazima pia tuwashikilie 
wanawake hawa, walikuwa wapi wakati mtoto kama huyu mdogo anatoweka 
nyumbani!, hata ndugu wengine pia watahojiwa," alisema Kamwela.
Kufuatia tukio hilo Kamwela alisema kuwa mama wa mtoto huyo ambaye 
ni mlemavu wa ngozi na bibi wa marehemu kwa pamoja watafikishwa 
mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
     SOURCE:
     NIPASHE
    
0 comments:
Post a Comment