Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mtoto Njiti akiwa amebebwa na mama yake.
WANAWAKE
 Mkoani Singida wamehimizwa kujenga tabia ya kuwakumbuka wanawake wenzao
 waliofungwa na walioko mahabusu gerezani ili waendelee kuaminiwa kuwa 
bado ni sehemu muhimu ya wanawake mkoani humu.
Wito 
huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake kanisa la
 Free Pentekoste church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida mjini, Lessi
 Jaredi muda mfupi baada ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa 
wanawake wanatumikia adhabu jela na wale walioko mahabusu katika gereza 
la wilaya ya Singida.Msaada huo ulikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku
 ya wananwake duniani.
Amesema
 wanawake waliopo magerezani, hawajapoteza utu wao na wala sio kwamba 
hawana msaada tena katika kuchangia maendeleo ya mkoa wa Singida na 
taifa kwa ujumla.
Baadhi ya watoto waliozaliwa kabla ya kufikia umri wa kuzaliwa (Njiti) ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida.
“Wanawake
 hawa ni wenzetu, ndugu zetu na watoto wetu, wapo gerezani kwa lengo la 
kusaidiwa kurekebisha baadhi ya mienendo na tabia zao tu.  Kwa hali 
hiyo, tunapaswa kuwapenda,kuwathamin na kuwajali, ili kuondoa uwezekano 
wao wasianze kuhisi kwamba, wametengwa au sio sehemu muhimu ya 
jamii”,alifafanua Mwenyekiti huyo.
Akisisitiza
 zaidi, Lessi amesema wanawake hao waliopo gerezani wakitembelewa na 
hasa na wanaweke wenzao na kukpewa misaada, kitendo hicho kitawatia moyo
 na kamwe hawatakata tamaa katika maisha yao.
“Nitumie
 fursa hii kuwahimiza wanawake wa jimbo la Singid mjini na wa mkoa wetu 
wa Singida kwa ujumla, tujenge utamaduni wa kuadhmisha siku ya wanawake 
duniani, kwa kuwatembelea wanawake wenzetu walioko magerezani, haspitali
 na wenye matatizo mbali mbali, ili makundi hayo yaweze kutembua kwamba 
tunayajali na kuyathamini”,amesema.
Katika
 hatua nyingine, Mwenyekiti huyo pia amewahimiza wanawake kuwatembelea 
wanawake walioko katika hospitali mbali mbali baada ya kujifungua watoto
 na hasa wale ambao watoto wao hawakufikisha umri wa kuzaliwa (njiti).
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida, Lessi Jaredi akimwombea mtoto Njiti ili Mungu aweze kumsaidia kuongeza uzito stahiki ambao utatoa fursa kwa wao kupewa ruhusa ya kurejea nyumbani kwao.
Amesema wanawake hao wanapaswa kufarijiwa mara kwa mara, sio tu na ndugu zao, bali na wanawake wengine kwa sababu wanalazwa muda mrefu wakisubiri watoto wao wafikishe uzito unaotakiwa.
“Sisi leo (jana 8/3/2014) wanachama wa UWW FPCT, tumetembelea wanawake sita walioko hospitali ya mkoa ambao wamejifungua watoto njiti. Tumebaini kwamba wana kazi kubwa ya kuhakikisha watoto wao njiti, wanafikisha uzito unaotakiwa. Kazi hiyo ambayo ni pamoja na kuwalisha kikamilifu ili kupata uzito stahili, inawalazimu kukaa hospitalini kwa mud amrefu”,alifafanua.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao licha ya kuhifadhiwa kwenye chumba chenye joto, pia wapo wengine ambao wanalazimika kupakatiwa kifuani na mama zao, ili kuuunganisha ngozi ya kifuani ya mama na ya mtoto, kwa lengo mtoto njiti,apate joto la mama yake aweze kukua na kuongeza uzito. Mhasibu wa Umoja wa wanawake wa kanisa Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida, Joyce Gunda,akikabidhi msaada kwa mgonjwa aliyelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida.Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu. Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (UWW-FPCT) Lessi Jaredi, akikabidhi msaada kwa mmoja wa wanawake waliojifungua watoto hawajafikia umri (Njiti) wa kuzaliwa.Msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka huu.
Picha na mtandao wa Singida yetu 





0 comments:
Post a Comment