Aliyekuwa
 tabibu msaidizi wa Dispensari ya Tumaini mjini Singida, (wa mbele) 
Godlisten Raymond (37) na mfanyabiashara wa mbuzi na biashara ya kusaga 
nafaka (wa tatu mbele) Adamu Shaban Hole (46) mkazi wa kijiji cha 
Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,wakisindikizwa na askari 
polisi kwenda gerezani kuanza kutumikia adhabu ya kila mmoja kifungo cha
 miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtoa mimba mwanafunzi na 
kusababisha kifo chake.
Mfanyabiashara
 wa Mbuzi na kusaga nafaka katika kijiji cha Kintandaa Adamu Shaban Hole
 (46) (mbele mwenye kofia baraghashia) na aliyekuwa tabibu msaidizi 
katika dispensari ya Tumaini mjini Singida, Godlisten Raymond (37) 
aliyefunika uso,wakisindikizwa gerezani kwenda kuanza kutumikia kifungo 
cha miaka 10 baada ya kutiwa hatiani na mahakama kuu kanda ya kati kwa 
kosa la kumpa mimba mwanafunzi na kuitoa na kusababisha kifo 
chake.Mwanafunzi huyo Hamida Athumani (16) alifariki dunia siku chache 
kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.(Picha na Nathaniel
 Limu).7
Na Nathaniel Limu, Singida
MAHAKAMA
 Kuu kanda ya kati iliyomaliza vikao vyake hivi karibuni mjini 
Singida,imewahukumu aliyekuwa tabibu msaidizi wa dispensari ya Tumaini 
Godlisten Raymond (37) adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya 
kupatikana na hatia ya kujaribu kutoa mimba kwa njia isiyo sahihi kwa 
 mwanafunzi na kusababisha kifo chake.
Mshitakiwa
 Godlisten anadaiwa kumtoa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi Kintandaa
 tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi, Hamida Athumani (16) septemba saba 
mwaka 2006 na alifariki dunia septemba 17 mwaka huo huo wa 2006, siku 
chache kabla ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Pia
 katika kesi hiyo,mfanyabiashara wa mbuzi na kusaga nafaka mkazi wa 
kijiji cha Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,Adamu Shabani Hole
 (46),naye amepewa adhabu ya kutumikia jela miaka 10 baada ya kupatikana
 na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi Hamida Athumani (16) na kisha 
kushiriki kutoa mimba hiyo na kusababishia kifo mwanafunzi huyo.
Ilidaiwa
 mahakamanai hapo kuwa mshitakiwa wa pili ambaye ni mfanyabiashara ya 
mbuzi,Adamu,katika kipindi hicho hicho,aliweza kumpa mwanafunzi mwingine
 Rukia Juma aliyekuwa akisoma darasa moja na Hamida (marehemu).
Rukia
 baada ya kutolewa mimba na washitakiwa,aliweza kulazwa katika hospitali
 ya mkoa mjini hapa,na aliweza kunusurika kufariki dunia baada ya 
kupatiwa matibabu.
Kabla
 ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwendesha mashitaka wakili wa serikali mkuu
 mfawidhi kanda ya Singida,Neema Mwanda,aliiomba mahakama hiyo itoe 
adhabu kali ya kifungo cha maisha jela kwa washitakiwa,ili iwe fundisho 
kwao na watu wengine wanaotarajia kuwatoa mimba wasichana wadogo na 
kisha kusababisha vifo vyao.
“Vitendo
 vya watu wazima kufanya mapenzi na wanafunzi na kisha kuwapa 
ujauzito,havikubaliki kabisa,kwa sababu zinaharibu maisha ya wanafunzi 
husika na wakati mwingine vinasababisha vifo.Pia madaktari na tabibu 
wasaidizi wenye tabia ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama,nao 
wanakwenda kinyume na sheria za taaluma zao”,amesema Mwanda.
Kwa
 upande wake wakili wa kijitegemea kutoka Dodoma mjini.Deus Nyabiri 
aliyekuwa anamtetea mshitakiwa wa kwanza,Godlisten,aliiomba mahakama 
hiyo impe adhabu nafuu mteja wake ikizingatia kuwa kosa hilo ni la 
kwanza kwake na pia anategemewa na familia yake na ya wazazi wake ambao 
kwa sasa,wana umri mkubwa.
Naye
 wakili wa kujitegemea wa mjini hapa,Raymond Kimu aliyekuwa akimtetea 
mshitakiwa wa pili,Adamu,aliiomba mahakama hiyo impe adhabu nafuu mteja 
wake na kiwezekana imwachie huru,kwa madai kuwa baada ya kuwapa mimba 
wanafunzi wawili waliokuwa darasa la saba,mke wake amemkimbia na familia
 yake imemtega.
Akitoa
 adhabu hiyo,jaji Cresentia  Makuru, amesema kwa mazingira ya 
kawaida,kosa walililofanya  washitakiwa,hawastahili huruma ya mahakama.
Amesema
 vitendo vya wasichana wadogo kupoteza maisha kwa kutolewa mimba kwa 
njia isiyo salama,licha ya kusababisha vifo vyao,pia vinachangia ndoto 
za wazazi kwa watoto wao,kupotea.
Aidha,jaji
 Makuru amesema katiba ya nchi,inatamka wazi kwamba uhai wa mtu ni 
lazima uheshimiwe na kulindwa.Hata sheria za kimataifa nazo zimetamka 
hivyo hivyo.
0 comments:
Post a Comment