Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
ZAIDI ya abiria 700 waliokuwa wakisafiri na treni ya abiria
wakitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam, wamekwama kwa siku mbili
wilayani Manyoni, baada ya treni ya mizigo kuanguka.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliofika eneo hilo jana, abiria
hao wamelilalamikia Shirika la Reli kutokana na kutokuwa na utaratibu
mzuri wa kusafirisha abiria wake pindi tatizo linapojitokeza.
Walisema walipofika Manyoni majira ya mchana, walielezwa kuwa treni
ya mizigo ilikuwa imeanguka kituo kinachofuatia cha Saranda, hivyo
wasubiri utaratibu.
“Lakini cha kushangaza mabasi ambayo yalikuwa yakiletwa na Shirika la
TRL yalikuwa machache kwa sababu abiria tulikuwa wengi,” alisema mmoja
wa abiria hao, Anton Beni.
Walisema kutokana na hali hiyo walilazimika kulala nje huku wakiwa na
watoto wadogo na wengine wagonjwa, kwani mabasi yalipokuwa yakifika
kuwachukua hakukuwa na utaratibu na kusababisha watu kugombea na kusema
hadi sasa baadhi ya abiria hawajui hatima yao ya kufika Dar es Salaam.
Meneja wa Kanda wa TRL kutoka Dar es Salaam, Philipo Rutizibwa,
alisema suala la abiria waliokwama Manyoni wameshafanya utarabu wa
mabasi na yameshaanza kuwachukua kuwapeleka wanakokwenda
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment