Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, Yahaya Nawanda.
Na Mwandishi wetu-Mo Blog
MKUU
wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, ameahidi kuishi kwa
siku tano katika nyumba za kabila la kisukuma kijiji cha Kizonzo tarafa
ya Shelui, ili kuhakikisha zoezi la kukusanya michango ya ujenzi wa
zahanati ya kijiji hicho linafanikiwa.
Nawanda
ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa
uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii
(CHF),uliofanyika kwenye kijiji cha Kizonzo.
Alisema
katika kipindi hicho atasimamia kwa karibu uchangiaji huo,ili ujenzi wa
zahanati hiyo uweze kufanyika mapema iwezekanavyo.
“Ninyi
ndugu zangu, mmekuwa mkipata taabu sana kufuata huduma ya afya kwenye
zahanati ya kijiji cha Mgongo kwa kutembea umbali wa kilomita nane
kwenda na kurudi. Akina mama wajawazito ndio wanaotaabika zaidi”,
alifafanua Nawanda
“Sasa
tunasema hatutakubali kabisa ninyi muendelee kutaabika kufuata matibabu
umbali mrefu kiasi hicho.Tunataka kipindi kifupi kijacho,matibabu
muyapate hapa hapa kijijini kwenu”.
Kutokana
na hali hiyo Nawanda amewataka wananchi kujiandaa mapema kwa zoezi hilo
la uchangiaji wa ujenzi wa zahanati yao unaotarajiwa uanza mapema
iwezekanavyo.
Kuhusu
mfuko wa afya ya jamii (CHF),mkuu huyo wa wilaya,alisema suala la
kujiunga na mfuko huo ni la lazima kwa madai kwamba afya bora ni mtaji
wa mwili wa binadamu ye yote.
“Wilaya
yetu ya Iramba, ni wilaya ya kwanza nchini kwa vituo vyake vyote vya
afya kuwa na dawa za kutosha wakati wote.Kwa hiyo mwanachama wa CHF,
nawahakikishia kuwa mtapata tiba wakati wote pindi watakapougua”,alisema
DC huyo.
Kwa
mujibu wa Dc Nawanda, kuku moja wa kienyeji mwenye thamani ya shilingi
10,000 tu, anatosha kugharamia ada ya kaya moja yenye mume, mke moja na
watoto wanane, kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka moja bila kuongeza
kiasi kingine cha fedha.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment