Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WIZARA ya Maji imetenga sh milioni 857 ili kukamilisha programu ya
maji vijijini na usafi wa mazingira katika vijiji 10 vya Tarafa ya
Kintinku wilayani Manyoni, Singida vilivyopo kwenye mradi wa Benki ya
Dunia.
Fedha hizo zilizotengwa kwenye mwaka wa fedha 2014/2015 ni sehemu ya
sh bilioni 1.5 kwa ajili ya tarafa hiyo kuwawezesha wakazi wa vijiji
hivyo kuwa na uhakika wa majisafi na salama kabla ya mwisho wa mwaka
2015.
Naibu Waziri wa Maji, Amosi Makala, alitoa ahadi hiyo alipozungumza
na wakazi wa Kata ya Chikuyu, Tarafa ya Kintinku kuhusu kumalizika kwa
tatizo la maji lililowakabili kwa muda mrefu.
Makala ambaye pia ni Mbunge wa Mvomero, alivitaja vijiji
vitakavyonufaika na mradi huo kuwa ni Kintinku, Lusilile, Ngaiti, Mvumi,
Maweni, Chilejeho, Mtiwe, Chikuyu, Mwiboo na Mbwasa.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa tarafa hiyo, Diwani wa Viti
Maalumu, Zinduna Abdallah (CCM), alimweleza naibu waziri huyo kwamba
tatizo la maji limeharibu ndoa za watu.
Mhandisi wa Sekretarieti ya mkoa huo, Yunusi Rugeyamu, alisema sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonyesha kuwa Singida ilikuwa na
wakazi 1,370,637 na kwamba hadi Desemba mwaka jana wakazi 656,932
waishio vijijini wanapata maji.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment