Sarafu mpya ya Tsh. 500/=
Baada ya kuonekana noti ya shilingi 500 ina na mzunguko mkubwa wa 
matumizi na inachakaa kwa haraka huku kiwango chake cha kuhimili 
mizunguko ni miezi sita, Benki kuu ya Tanzania (BOT) inatarajia kubadili
 noti hiyo na kuifanya sarafu.
Sarafu hiyo ya 500 inatarajiwa kutambulishwa na kuanza kutumika July 
2014 ikienda sambamba na kipindi cha mwaka huu wa fedha ambapo unaambiwa
 hii sarafu ikishatoka inatarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya 
miaka 20 na kubaki na ubora wake uleule, yani ni imara kuliko noti.
Noti ya 500 inayotumika sasa
Afisa mkuu wa benki kitengo cha idara kurugenzi za kibenki Patrick Fata 
ameongea na millardayo.com na kusema “Tunafanya hivi kwasababu noti ya 
500 inachakaa haraka kulinganisha na mzunguko wake na kuwafikia watu 
wengi pia huchakaa haraka kutokana na mzunguko wa kushikwa na watu 
wanaofikia mpaka milioni moja kwa siku, hiyo ni idadi kubwa kuliko ya 
wanaoshika noti ya elfu 10 kwa siku’

0 comments:
Post a Comment