ALAT MKOANI SINGIDA WATAKIWA KUKUSANYA MAPATO YA ADA ZA LESENI



Na SingidaYetu.Blogspot.com

Wajumbe wa  jumuiya ya tawala za mikoa Tanzania  ALAT  mkoa wa Singida wametakiwa kuonyesha  uwezo wa kukusanya  mapato yanayotokana na Ada za lesen kwa ukamirifu  ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone wakati wa ufunguzi wa Kikao cha ALAT mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa parokia ya kanisa katoliki mjini Singida

Dr. Kone amesema ada za lesen zikikusanywa  kwa ukamilifu serikal itaongezea halmashauri za mkoa wa Singida wigo mpana wa vyanzo katika halmashauri zote
Amesema kwa kutumia fursa hiyo ya makusanyo kutasaidia kuwa na matokeo chanya kwa kuibua,kukusanya kusimamia na kufuatilia mapato ya halmashauri.

SINGIDA YAAGIZA DOZI MPYA CHANJO YA UGONJWA WA KIDERI

WILAYA ya Iramba mkoani Singida imelazimika kuagiza  zaidi ya dozi  laki nne za chanjo ya ugonjwa  wa kideri moja kwa moja toka kiwandani, kwa ajili ya kusambaza  kwa wafugaji wa kuku.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika kuwa dawa na chanjo nyingi zinazonunuliwa na   wananchi kwenye maduka binafsi ya kilimo na mifugo zinakuwa zimechakachuliwa na kusababisha kuku kufa.
Akizungumza kwenye  mafunzo ya ufugaji  bora wa kuku, Mkuu wa Wilaya  hiyo Yahaya Nawanda amesema baada ya kubaini tatizo katika chanjo hizo, wameona  vyema kuagiza moja kwa moja toka  kiwandani zinakotengenezwa na kuzimbaza kwa wananchi  wanaofuga kuku Vijijini.
Bwana Nawanda amesema  tayari  mpango huo umeanza kutekelezwa  na  dozi hizo za chanjo zaidi ya laki nne zinatarajiwa kuwa zimewasili  katika Wilaya ya Iramba kabla  ya mwisho wa mwezi huu.
Ufugaji wa kuku wa asili ni moja shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Singida ambapo inakadriwa kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana zaidi ya kuu milioni mbili walikuwa wanafugwa.

UCHAFU MJINI SINGIDA WAWA KERO

                                                     (Picha zote kutoka maktaba)
Kuongezeka kwa idadi ya watu katika kata ya Mandewa Manispaa ya Singida kumesababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa taka laini na ngumu katika kata hiyo na maeneo jirani.
Mwenyekiti wa kamati ya usafi na mazingira kata ya Mandewa Bw. Elifuraha Mgoma amesema hayo muda mfupi baada ya kumaliza shughuli za kufanya usafi eneo la Ginery manispaa ya Singida.
Amesema hivi sasa kunaongezeko watu lilochangiwa na taasisi za elimu kama vile vyuo, pamoja na shule jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa wingi wa uzalishaji wa taka katika maeneo ambayo watu hao wanaishi.
Amesema jitihada za haraka zinahitajika ili kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kujenga guba la kukusanyia uchafu kwa lengo la kuepukana magonjwa ya miripuko yanayoweza kutokea kwa sababu ya kuzagaa kwa taka

PICHA NA MTANDAO WA SINGIDA

MOHAMMED DEWJI AMONG TWO YOUNGEST BILLIONAIRES ON CONTINENT

Mohamed deji3
MeTL Group CEO Hon.Mohammed Dewji.
Africa boasts 55 billionaires from 10 countries
Africa, the world’s fastest growing emerging market, is now home to 55 billionaires, with an average net worth of $2.6bn.

By Rebecca Burn-Callander, Enterprise Editor - The Telegraph
Africa is now home to 55 billionaires, up from previous estimates of 16-25 billionaires, new research has found. These super rich are worth a combined total of $143.88bn (£89.27bn).
The UK, in contrast, is home to 84 billionaires, worth a nearly £250bn, according to the 2013 Sunday Times Rich List.

With 55 billionaires, Africa is comparable to Latin America, which has 51 at last count (Forbes). However, Africa has some way to go if it's to top the super-rich tally in Asia, which is home to 399 billionaires as of 2013.

The new study, undertaken by African business magazine and news service Ventures Africa, is the most extensive list ever compiled, claims founder Chi-Chi Okonjo. It reveals the “true wealth” of Africa’s richest people, he said. The richest man in Africa is cement, sugar and flour tycoon Aliko Dangote. The Nigerian is worth $20.2bn. This figure is slightly up on Forbes’ estimation of $16.1bn for his wealth as of March this year.

In second place, South African financier Allan Gray holds assets worth at least $8.5bn.
Third on the list, Nigerian Mike Adenuga, with operations in the oil and telecoms industries, has an estimated fortune of $8bn.
Africa’s wealthiest woman, Nigerian oil tycoon Folorunsho Alakija, is worth $7.3bn.
The median age of Africa’s billionaires stands at 65 years old, with the youngest billionaires both at 38. These young guns are Tanzanian Mohammed Dewji, head of the largest textile manufacturer in sub-Saharan Africa, and Nigerian oil trader Igho Sanomi.

The oldest billionaires are Manu Chandaria, a Kenyan industrialist, and Mohammed Al-Fayed, the Egyptian property tycoon and Harrods boss, who are both 84. Nigeria, South Africa and Egypt have the most billionaires with 20, nine and eight respectively. In total ten African countries are represented on the list.

According to Ventures Africa, there are a large number of African billionaires on its list whose fortunes have never been accurately calculated before including: Strive Masiyiwa (Zimbabwe, $1.46 billion); Abdulsamad Rabiu (Nigeria, $1.4 billion); Aziz Akhannouch (Morocco, $1.39 billion); Jide Omokore (Nigeria, $1.32 billion); and Bode Akindele (Nigeria, $1.19 billion).
“This list is a tribute to the entrepreneurial heartbeat within Africa,” said Mr Okonjo.

The report credits the surge in energy prices over the last decade for the increase in billionaires. The price of oil topped $100 a barrel this year, up from $20 a barrel in early 2000. The list was been compiled using financial reports, by tracking equity holdings around stock markets and identifying specific shareholding structures in large, privately-held companies. The results have been corroborated with investment bankers, realtors and financial analysts to determine proper values for companies, real estate and other assets, such as art collections, jets, yachts and jewellery.

MOHAMMED DEWJI AMONG TWO YOUNGEST BILLIONAIRES ON CONTINENT

Mohamed deji3
MeTL Group CEO Hon.Mohammed Dewji.
Africa boasts 55 billionaires from 10 countries
Africa, the world’s fastest growing emerging market, is now home to 55 billionaires, with an average net worth of $2.6bn.

By Rebecca Burn-Callander, Enterprise Editor - The Telegraph
Africa is now home to 55 billionaires, up from previous estimates of 16-25 billionaires, new research has found. These super rich are worth a combined total of $143.88bn (£89.27bn).
The UK, in contrast, is home to 84 billionaires, worth a nearly £250bn, according to the 2013 Sunday Times Rich List.

With 55 billionaires, Africa is comparable to Latin America, which has 51 at last count (Forbes). However, Africa has some way to go if it's to top the super-rich tally in Asia, which is home to 399 billionaires as of 2013.

The new study, undertaken by African business magazine and news service Ventures Africa, is the most extensive list ever compiled, claims founder Chi-Chi Okonjo. It reveals the “true wealth” of Africa’s richest people, he said. The richest man in Africa is cement, sugar and flour tycoon Aliko Dangote. The Nigerian is worth $20.2bn. This figure is slightly up on Forbes’ estimation of $16.1bn for his wealth as of March this year.

In second place, South African financier Allan Gray holds assets worth at least $8.5bn.
Third on the list, Nigerian Mike Adenuga, with operations in the oil and telecoms industries, has an estimated fortune of $8bn.
Africa’s wealthiest woman, Nigerian oil tycoon Folorunsho Alakija, is worth $7.3bn.
The median age of Africa’s billionaires stands at 65 years old, with the youngest billionaires both at 38. These young guns are Tanzanian Mohammed Dewji, head of the largest textile manufacturer in sub-Saharan Africa, and Nigerian oil trader Igho Sanomi.

The oldest billionaires are Manu Chandaria, a Kenyan industrialist, and Mohammed Al-Fayed, the Egyptian property tycoon and Harrods boss, who are both 84. Nigeria, South Africa and Egypt have the most billionaires with 20, nine and eight respectively. In total ten African countries are represented on the list.

According to Ventures Africa, there are a large number of African billionaires on its list whose fortunes have never been accurately calculated before including: Strive Masiyiwa (Zimbabwe, $1.46 billion); Abdulsamad Rabiu (Nigeria, $1.4 billion); Aziz Akhannouch (Morocco, $1.39 billion); Jide Omokore (Nigeria, $1.32 billion); and Bode Akindele (Nigeria, $1.19 billion).
“This list is a tribute to the entrepreneurial heartbeat within Africa,” said Mr Okonjo.

The report credits the surge in energy prices over the last decade for the increase in billionaires. The price of oil topped $100 a barrel this year, up from $20 a barrel in early 2000. The list was been compiled using financial reports, by tracking equity holdings around stock markets and identifying specific shareholding structures in large, privately-held companies. The results have been corroborated with investment bankers, realtors and financial analysts to determine proper values for companies, real estate and other assets, such as art collections, jets, yachts and jewellery.

Timu ya Minga bingwa mpya kombe la MO 2013/2014

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP. Geofrey Kamwela (wa kwanza kulia) wakifurahia jambo na OCD wa wilaya ya Singida, Mohammed Mwinyipembe (katikati) na msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini, Duda Mughenyi wakati mechi ya fainali ya ligi kombe la MO
 Msaidizi wa mbunge wa jimbo la Singida mjini, Duda Mughenyi akitoa taarifa ya ligi ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Dewji iliyomalizika mwishoni mwa Juma.
 Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP.Geofrey Kamwela akimkabdhi kombe la ubingwa wa ligi ya Mo, kapteni wa timu ya Minga ya manispaa ya Singida, Shaban Juma.
 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Minga wakifurahia baada ya kunyakua ubingwa wa ligi ya kombe la MO.
Baadhi ya wapenzi wa soka waliokuwa wakifuatilia mechi ya fainali ya kombe la mbunge wa Singida mjini,Mohammed Dewji iliyofanyika mwishoni mwa Juma kwenye uwanja wa Namfua.
Timu ya soka ya kata ya Minga Manispaa ya Singida imetawazwa mabingwa wa kombe la Mbunge wa Jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji (MO) kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 baada ya kuichapa Mungumaji goli 2-1 kwenye mechi kali na ya kusisimua iliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua jijini Singida.
Hata hivyo mechi hiyo ilivunjika dakika tano kabla ya kuisha baada ya timu ya Mungumaji kugomea kuendelea na mechi hiyo kwa madai kuwa mwamuzi wa mchezo huo alikuwa hawatendei haki katika maamuzi yake.
Mechi hiyo ilivunjika baada ya Mwamuzi Sarah Bogi kuwatoa nje kwa kadi nyekundu Yahaya Juma wa Minga na Hamisi Hamisi wa Mungumaji kwa kitendo cha cha kupigana uwanjani.
Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na wapenzi wengi zaidi wa soka ikilinganishwa na mechi zote zilizochezwa kwenye ligi hiyo iliyoanza septemba mosi mwaka huu magoli mawili ya Minga yalifungwa na Shaban Juma,wakati lile la kufutia jasho la Mungumaji lilifungwa na Hamisi Hamisi.
Mgeni rasmi katika mechi hiyo ya fainali alikuwa Kamanda Polisi Mkoa wa Singida, ACPGeofrey Kamwela amesema wachezaji wa timu hizo zilizofanikiwa kucheza fainali wameonyesha vipaji vya hali ya juu.
“Kwa kweli vijana wameonyesha wazi kama wataendelezwa wanaweza kufika mbali katika mchezo wa soka, wamenivutia mno na mimi nitaangalia uwezekano wa kuendeleza mchezo wa soka ili vijana waweze kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao kwa manufaa yao na ya mkoa pia”,amesema Kamwela.
Kwa upande wake Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Duda Mughenyi amesema MO ameanza kufadhili ligi hiyo toka mwaka 2003 hadi sasa.
Amesema lengo kuu la ligi hiyo limebaki kuwa lile lile la kuibua vipaji ili pamoja na mambo mengine vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.
“Nitumie fursa hii kuwaomba na wadu wengine wa michezo kufufua na kuendeleza michezo mbalimbali katika Manispaa ya Singida ili vijana na watu wengine waweze kuonyesha vipaji vyao kwa manufaa ya wahusika,wilaya na Mkoa wa Singida”,amesema Duda.
 
NA BLOG YA SINGIDA

Kampuni ya madini ya Shanta yatumia shilingi 23.6 milioni kugharamia ujenzi wa matundu ya choo

DSC03496
Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya, akizungumza kwenye mahafali ya 48 ya shule ya msingi ya Mang’onyi.Wa kwanza kushoto ni meneja mahusiano wa kampuni ya madini ya Shanta na anayefuatia ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ya Mang’onyi, Andrea Andalu.
DSC03467
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua choo chenye matundu 40 cha shule ya msingi Mang’onyi kilichojengwa na kampuni ya Shanta.Wa kwanza kulia ni afisa elimu wilaya ya Ikungi Gerald Kivuyo.Wa kwanza kushoto ni meneja mahusinao wa kampuni ya madini ya Shanta,Credo Simbaye na anayefuata ni mkuu wa shule ya msingi ya Mang’onyi, Adamu Mwekwa.
DSC03499
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Manju Msambya akigawa vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.
DSC03447
Jengo la ofisi ya kijiji cha Mang’onyi kilichojengwa kwa msaada ya kampuni ya madini ya Shanta.
DSC03449
Jengo la kituo cha kisasa cha polisi kata ya Mang’onyi kinachoendelea kujengwa kwa msaada ana kampuni ya madini ya Shanta.Anayeonyesha jengo hilo la kituo cha polisi,ni meneja Ardhi na Makazi wa kampuni ya madini, Elisante Kamuya.
DSC03451
Vyumba vya Choo vilivyojengwa na Kampuni ya madini ya Shanta.
DSC03452
Jengo la choo cha shule ya msingi cha zamani cha shule ya msingi Mang’onyi wilaya ya Ikungi ambacho hakifai kwa matumizi tena.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Mang’onyi
Kampuni ya madini ya Shanta Singida imetumia zaidi ya shilingi 23.6 milioni kugharamia ujenzi wa choo cha matundu 40 katika shule ya msingi Mang’onyi jimbo la Singida mashariki.
Hayo yamesemwa juzi na Meneja Mahusiano wa kampuni ya madini Shanta,Credo Simbaye wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya choo hicho iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mang’onyi.
Amesema kwamba uamuzi wa kampuni ya Shanta kutoa msaada huo wa ujenzi wa choo ni kuinusuru shule hiyo kufungwa kutokana na kukosa choo.
“Baada ya mamlaka husika kutaka kuifunga shule hii kongwe kwa muda usiojulika kutokana na kukosa kabisa choo kamati ya shule ilileta ombi kwetu tusaidie kuijengea choo cha matundu 40 ili isifungwe na wanafunzi zaidi ya elfu moja wakakosa masomo ombi hilo tulilipokea kwa mikono miwili”,alisema Simbeya
Meneja Mahusiano huyo amesema pamoja na Shanta bado haijaanza shughuli zake za uchimbaji madini iliona upo umuhimu mkubwa kujenga choo kwa shule hiyo ili wanafunzi wasikatishe masomo kwa tatizo la choo.
“Unapowekeza  katika biashara ya madini au maliasili yo yote ile kimsingi unakuwa umekubali pia kuwa mdau wa maendeleo ya wananchi katika eneo husikajukumu mojawapo ni kuhakikisha kwamba msukumo wa maendeleo yanayotarajiwa unapata nguvu za pamoja”amesema Simbaye.
Aidha amesema pia hivi sasa wapo kwenye maandalizi ya kuchimba kisima kirefu cha maji kitakachosaidia kupunguza uhaba mkubwa wa maji unaochangia wakazi wa kata ya Mang’onyi kuchangia maji na mifugo.
“Kama nilivyosema awali kwamba Shanta haijaanza kuchimba madini lakini hilo halijazuia kampuni kutoa misaada ili kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata ya Mang’onyi.
Simbaye amesema kwa sasa wanajenga chumba cha darasa katika shule ya msingi Mlumba kituo cha kisasa cha polisi kata ya Mang’onyi,vijana 210 wamepata ajira za muda na kampuni imeendelea kutoa magari kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa kuwapeleka kituo cha afya Ikungi na zahanati ya kijiji cha Mwau.
“Wito wangu kwa wananchi wa wilaya ya Ikungi na hususan wa kata ya Mang’onyi ,nawaomba waamini kwamba,mradi wa dhahabu wa Shanta Singida,utakapoanza utafungua ukurasa mpya wa maendeleo kwa wilaya ya Ikungi na mkoa wa Singida,hivyo hawana budi kuunga mkono”,alisema meneja Simbaye.

chanzo: Mo Blog

Singida kujenga machinjio ya kuku wa asili

WILAYA ya Iramba mkoani Singida inatarajia kuanzisha machinjio ya kuku wa asili ifikapo Julai mwakani.
Mkuu wa wilaya  hiyo bwana Yahaya Nawanda amebainisha hayo Mjini Kiomboi wakati akifungua   mafunzo ya siku mbili juu ya ufugaji kuku kisasa na kuanzisha SACCOS ya  wafugaji kuku
Amesema lengo la machinjio hayo ya kisasa yaliyopangwa kujengwa katika mji wa Misigiri ni kuhakikisha  kuwa kuku wanaozalishwa wanaongezwa thamani kwa kuchinjwa na kusindikwa ili kukidhi mahitaji ya soko badala ya kusafirishwa hai kwa adha kubwa na wengine kufa njiani.
Amesema uamuzi  wa kujenga machinjio  hayo  umefikiwa baada ya kubaini kuwa licha ya ufugaji wa kuku wa asili kuwa moja ya shughuli kuu za kiuchumi mkoani  Singida, kumekuwepo na changamoto mbalimbali.
Amesema miongoni mwa changamoto hizo ni  pamoja na ukosefu wa soko la uhakika na bei nzuri,  uhaba wa madawa na vifo  vinavyotokana na magonjwa na mazingira magumu ya usafirishaji.
Amesema kujengwa kwa machinjio hayo na kunzishwa kwa soko la kuku  pamoja na kituo cha kutoa elimu juu ya ufugaji wa kuku kisasa,  vitasaidia kuwaingiza wananchi kufuga kuku kibiashara ili kujikomboa kiuchumi.
 Inakadiriwa  kuwa zaidi ya kuku milioni  mbili wa  asali  wanafugwa  mkoani Singida.

Bilioni 6.4 zatumika ujenzi wa barabara Singida


ZAIDI  ya shilingi  bilioni 6.4 zimetumika kwa ajili ya shughuli  za  matengenezo ya barabara kuu, mkoa na madaraja  katika mkoa wa  Singida katika kipindi cha kuanzia  Januari hadi  Juni mwaka huu..

Kaimu meneja wa wakala wa baraara TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi Yohannes Mbegalo, amebainisha hayo jana wakati akizungumza kwenye kikao cha 35 cha bodi ya barabara.

Mhanadisi  Mbegalo amesema  kuwa  fedha hizo zimetumika  kwa  ajili ya kugharamia  shughuli  za matengenezo ya kawaida kwa upande wa barabara za lami na changarawe zilizopo  mkoani Singida.

Amebainisha baadhi ya shughuli zilizofanyika kuwa ni pamoja na  matengenezo ya sehemu korofi, matengenezo ya vipindi maalum pamoja na matengenezo ya  kawaida na  kujenga makalvati.

Wakala wa barabara mkoa wa Singida,unahudumia jumla ya kilomita 1,689.5 za barabara kuu na zile za mkoa.

Kati ya hizo,kilomita 367.9 ni za lami sawa na aslimia 21.8 na sehemu iliyobaki yenye urefu wa kilomita 1,321.6 sawa na asilimia 78.3 ni za barabara za changarawe  na udongo.


Wanafunzi wabuni kifaa cha kumwagilia


Wanafunzi wawili Fideli Samwel na Jafari Ndagula kutoka shule ya sekondari Ilongero, iliyopo mkoani Singida, wameibuka washindi katika mashindano ya sayansi kwa vitendo iliyoshirikisha mikoa 18 nchini.

Mashindano hayo yalishirikisha wanafunzi 120 kutoka  shule za sekondari 60 pamoja na walimu wao wa sayansi, kwa ajili ya kuonyesha ubunifu na vipaji vya kisayansi ili kuzalisha wataalamu wengi nchini.

Ndagula alizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kutangazwa kuwa mshindi, alisema kubuni kifaa cha umwagiliaji, hawakuwa na uhakika wa kushinda kwenye maonyesho hayo na kwamba wanamshukuru Mungu kuwafanikisha.

Kifaa hicho kinatumika kama pampu ya kusukuma maji ambayo ina mipira maalumu inayoweza kumwagilia shamba au bustani.

“Unajua mashindano yalikuwa magumu, karibu washiriki wote wamejiandaa vizuri walibuni vifaa ambavyo vinahitajika ndani ya jamii, hivyo tusikate tamaa bali kila mmoja asonge mbele,” alisema. 

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema katika kuhakikisha vipaji hivyo vinaendelezwa Serikali imetenga Sh. bilioni 26 kwa ajili ya ukarabati wa maabara zake na kujenga zingine kwenye shule zote nchini.

Alisema mpango huo utasaidia kuongeza kasi kwa wanafunzi kujifunza masomo ya sayansi kwa kuwa na maabara za kutosha na za kisasa, pia serikali inajenga mtandao wa ufundishaji (ICT) utakaounganishwa kwenye Mkongo wa Taifa na mwalimu kufundisha kimtandao.

Naye Balozi wa Ireland nchini, Flonnual Gilsenan, alisema Serikali yake itaendelea kulidhamini Jukwaa la vijana wanasayansi Tanzania (YST) ili kuhakikisha linatimiza malengo ya kuzalisha wataalamu.

“Nitaendelea kushirikiana na Serikali yangu kuendeleza ubunifu wa vijana wa Kitanzania kupitia YST, pia naishukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wao,”alisema.

Naye Mkurugenzi wa YST, Gozbert Kamugisha, alisema maonyesha hayo yanadhihirisha ubunifu wa hali ya juu kwa Taifa kupata wataalamu wa kutosha, ikiwa fursa hiyo itatumika kuboresha kazi zao.

Alisema YST inasaidia kuwatangaza wasayansi miongoni mwa vijana na kuwapa moyo wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili katika maisha ya kila siku.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza alipata Sh. milioni moja, medali, kikombe na tiketi ya kwenda kushiriki mashindano ya wanasanyansi vijana nchini Ireland.
 
CHANZO: NIPASHE




Hii Hatari :Vyandarua vyatumika kuezeka vyoo badala ya kukinga Mbu!

DC
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Edward Ole Lenga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinampundu mara baada ya kukabidhiwa Zahanati na nyumba mbili za mganga na shirika moja lisilo la kiserikali la HAPA,hafla hiyo ilifanyikajuzi kijijini hapo.
SIMAVI
 Ni Mwakilishi wa shirika la SIMAVI kutoka nchini Uholanzi Lieke Ongering akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wake kwa ushirikiano na shirika la HAPA Singida kukamilisha mradi wa ujenzi wa Zahanati na nyumba mbili za mganga kijiji cha Kinampundu takribani umbali wa kilomita 70 kutoka mjini Singida.
NAPIMA
Ni mmoja wa kinamama wajawazito akipimwa uzito na mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ole Lenga mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya zahanati hiyo, anayeshuhudia kipimo hicho ni mhasibu mkuu wa shirika hilo Noel Makyao.
VIFAA
Mkurugenzi wa HAPA Davd Mkanje  (Kulia) kimkabidhi DC wa Mkalama Ole Lenga baadhi ya vifaa vya kutolea huduma kwenye Zahanati hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mradi huo.
SELEBUKA
Ni baadhi ya wageni kutoka Mataifa mbalimbali nje ya nchi wakicheza muziki na wananchi wa kijiji cha Kinampundu mara baada ya kukabidhiwa mradi huo wa afya ya uzazi wa mama na mtoto.
UKAGUZI
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ole Lenga, kushoto mwenye suti, mwakilishi wa SIMAVI, Lieke, MMkurugenzi wa shirika la HAPA, Davd Mkanje na mhasibu mkuu wa shirika hilo Noel Makyao wakifurahia pamoja na wananchi mara baada ya kukabidhi mradi huo.
Na Hillary Shoo, MKALAMA.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida ameonya tabia ya baadhi wananchi kuezekea kwenye vyoo vyandarua vya kujikinga na mbu wa malaria.
Onyo hilo limetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkuu huyo wa Wilaya, Edward ole Lenga wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinampundu muda mfupi baada ya kukabidhiwa Zahanti ya kijiji na shirika la HAPA.
Alisema imezuka tabia ya wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa matumizi yasiyo rasmi ikiwa na pamoja na wengine kuvifanya kama mabanda ya kuhifadhi vifaranga vya kuku.
“Hii ni aibu, wenzetu wanatupatia vyandarua  ili tusipate malaria, nyie mnatumia kuezeka vyoo kwa kweli hii ni aibu kubwa sana na mimi nimetembea vijijini na kujionea hili, na kwa kweli atakayekamatwa atakiona cha moto.” Alisema Dc Lenga kwa masikitiko.
Aidha alisema serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kuagizi vyandarua hivyo kwa ajili kujikinga na mbu wa malaria huku wananchi wakiziona kana kwamba hazina msaada na kuzitumia kama kinga kwenye vyoo.
“Hivi chandarua kukiezekwa kwenye choo si mtu unaonekana tu , acheni hii tabia chafu, nimeunda kikosi kila kijiji atakayebainika kufanya hivyo akamatwe na kuletwa kwangu mimi nitamshughulikia ipasavyo.” Alisisitza Ole Lenga.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi wa Wilaya hiyo wanaoishi maeneo ya mijini kuja nyumbani na kujenga nyumba na vyoo bora.

Kwa hisani ya Mo Blog

WFP watoa msaada wa pampu za maji zenye thamani Tsh 94 millioni mkoani Singida


DSC02783
Mkuu wa Ofisi ndogo ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dodoma, Nima Sitta akihimiza utunzaji wa matenki ya kuvunia maji ya mvua yaliyojengwa katika shule za msingi wilaya ya Singida na Ikungi. Shirika la WFP limetoa shilingi 95,271,600 kugharamia ujenzi wa matenki hayo.(Picha  na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Shirika lisilo la kiserikali la Mpango wa chakula duniani (WFP) limetoa msaada wa pampu 210 za maji zenye thamani ya zaidi ya shilingi 94 milioni kwa shule za msingi na vikundi mbalimbali mkoani Singida.
Pampu hizo ni kwa ajili ya kilimo cha umwangiliaji bustani.
Hayo yamesemwa juzi na Mkuu wa Ofisi ndogo ya WFP Dodoma Nima Sitta,wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matenki 12 ya kuvunia maji ya mvua yaliyojengwa kwenye shule sita za wilaya ya Singida na wilaya ya Ikungi.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Igaruri wilaya ya Singida.
Alisema lengo kuu la msaada huo wa pampu za maji,ni kila shule za msingi na vikundi vya vijana,kuanzisha kilimo cha umwangiliaji maji bustani.
Nima alisema kila shule ya msingi yenye chanzo cha maji,itapatiwa pampu si chini ya mbili,wakati vikundi vya vijana waliomaliza elimu ya msingi na wale waliomaliza kidato cha nne,watapatiwa si chini ya pampu tatu.
“Kwa upande wa vijana,kila kikundi kinatakiwa kumiliki ekari sisizopungua tatu na wawe wamejipanga vizuri,shule za msingi zimepewa sharti la kuwa na shariti la kumiliki ekari mbili.Hivi sasa tunaendelea kuzizungukia shule ili zile zenye sifa,ziweze kukabidhiwa pampu mapema iwezekanavyo”alifafanua Nima.
Katika hatua nyingine,Nima alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika lisilo la kiserikali la SEMA la mjini Singida, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa matenki ya kuvunia maji na inayofanana na thamani ya fedha zilizotumika .
“Kwa kweli SEMA kazi yao ni nzuri mno,wametekeleza kwa kiwango cha juu yale yote ambayo yapo kwenye mkataba na kufanya mazuri zaidi baadhi ya shughuli ambazo hazipo kwenye mkataba.Nisema tu kwamba kazi ya SEMA,inapaswa kuigwa na wajenzi wengine kwa maendeleo ya wananchi”,alisema.

Mkandarasi atishia kujitoa ujenzi wa barabara

KAMPUNI ya China ya Sinohydro imetishia kusimamisha ujenzi wa barabara ya lami ya Manyoni- Itigi mkoani Singida hadi Chaya mpakani mwa Tabora kutokana na kuidai Serikali zaidi ya Sh bilioni 14.7. Madai hayo ni sehemu ya gharama za ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 89.3 kwa kazi ambayo imekwishafanyika.

Hali hiyo inatajwa kuwa moja ya sababu za utekelezaji wa mradi huo kuwa nyuma kwa zaidi ya miezi sita sasa kutokana na mkandarasi kukabiliwa na uhaba wa fedha.

Mkandarasi mshauri wa mradi huo Nicholas Geyer kutoka Ireland, alisema kutokana na madai ya fedha kwa muda mrefu bila mafanikio, shughuli hiyo inaweza kusimamishwa wakati wowote.

Alisema hatua hiyo itakachelewesha zaidi ujenzi na kuigharimu Serikali kwa kulazimika kulipa fidia kwa mujibu wa sheria za mikataba.

Hata hivyo, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Singida, Yustaki Kangole alisema anaamini Serikali italipa fedha hizo kumuwezesha mkandarasi kuendelea na ujenzi.

Alisema huo ni sehemu tu ya miradi mingi nchini inayodaiwa zaidi ya Sh bilioni 300.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, aliyetembelea ujenzi wa barabara hiyo alisema na kuchelewa suala kubwa ni kuzingatia ubora.

Ujenzi wa barabara ya lami ya Manyoni-Itigi-Mkoani Singida hadi Chaya mpakani mwa Tabora unaogharimu zaidi ya Sh bilioni 100 ulitarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu kwa mujibu wa mkataba.
Chanzo: Mtanzania

Halmashauri ya Singida yakusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 22 kutoka vyanzo yake mbalimbali.

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Jumanne Mnyampanda (katikati) akiongoza kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wanancvhi mjini Singida. Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Singida Hamisi Mumbee na kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Singida Illuminata Mwenda.
 Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kikao cha baraza la madiwani. Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.
Mwenyekiti wa huduma za jamii katika halmashauri ya wilaya ya Singida na diwani (CCM) wa kata ya Msange Elia Digha, akichangia hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Singida.
Halmashauri ya wilaya ya Singida imekusanya mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali zaidi ya shilingi bilioni 22.9 kati ya Julai mwaka jana na Juni mwaka huu.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Illuminata Mwenda amesema hayo wakati  akitoa taarifa yake ya mapato na matumizi kwenye kikao cha baraza la madiwani, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.
 Amesema makusanyo hayo ya mapato ni sawa na asilimia 78 ya lengo la kukusanya shilingi 29,583,444,380 kwa mwaka huo wa fedha.

 Mwenda amesema kuwa vyanzo vya ndani vya mapato, walikusanya zaidi ya shilingi..........
419,000,000 sawa na aslimia 42 ya lengo la kukusanya shilingi 1,004,817,000.
Mkurugenzi huyo amesema serikali  kuu imewapa ruzuku ya kulipia mishahara zaidi ya shilingi 13.8 bilioni na ruzuku nyingine ya zaidi ya shilingi 1.5 bilioni kwa ajili ya matumizi yasiyo ya mishahara.
 Katika hatua nyingine, kikao hicho kimeagiza mkaguzi wa mahesabu wa ndani afanye ukaguzi wa vitabu vya kukusanyia mapato ya ndani kwa watendaji wote wa kata.

 Vile vile mkaguzi huyo, amkague kwa makini Afisa mapato wa halmashauri hiyo anayehusika na kutoa vitabu vya kukusanyia mapato.


 Aidha, kikao hicho kimemwagiza mkaguzi huyo kufanya ukaguzi zaidi kwa watendaji wa kata ya Merya, Itaja, Mudida na Ikhanoda ili kubaini tuhuma zinazowakabili.
Chanzo. Blog ya Singida

Kijana wa kiume mkoani Singida aingiliwa kinyume na maumbile baada ya kulewa pombe na kupoteza fahamu.

KAMWELA
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kijana mmoja mkazi wa Kibaoini Singida mjini, kulawitiwa na rafiki yake baada ya kulewa pombe ya viroba aina ya jogoo.(Picha na Nathaniel Limu).
‘Ulevi noma’ hiyo imedhihirika baada vijana wawili wa kiume marafiki kunywa pombe nyingi na kuepelekea mmoja amwingilie kimwili kinyume na maumbile rafiki yake kipenzi.
Inadaiwa Athumani Juma mkazi wa Kibaoni alimwingilia kimwili kinyume na maumbile rafiki yake wa kiume mwenye umri wa miaka 26 (jina tunalo).
Kamanda wa polisi wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la aina yake, limetokea Agosti 27 mwaka huu saa tatu usiku eneo la soko la Kibaoni kata ya Kindai mjini Singida.
Amesema siku ya tukio, marafiki hao walikutana dukani ambapo mtuhumiwa Athumani alinunua viroba vinne aina ya jogoo, huku muathirika akinunua viroba tisa.
Kamanda Kamwela amesema baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, muathirika alitangaza kuwa amelewa na hivyo kila mmoja arejee  nyumbani kwao.
Kamanda kamwela amesema “Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia rafiki yake Athumani kuwa amwache hapo ili aweze kupumzika kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana, lakini ghafla alianguka chini na kisha kuzirai na kupoteza fahamu”.
Amesema kuwa baada muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa Athumani alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili rafiki yake kinyume na maumbile.
Amesema wapita njia waliweza kushuhudia  Athumani akiendelea na unyama wake huo dhidi ya rafiki yake, lakini walipojaribu kumkamata, aliweza kuwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.
Kamnda huyo ameongeza kuwa “Raia wema walimbeba muathirika na kumpeleka hadi nyumbani kwao na baadae aliweza kupata  fahamu na ndipo aliposikia maumivu makali kwenye sehemu yake ya haja kubwa”.
“Baada ya muathirika kusikia maumivu makali, alikimbizwa hospitali ya mkoa na baada ya uchunguzi, alibainika ameharibiwa  vibaya sehemu yake ya siri ya kutolea haja kubwa”.
Kamwela amesema kwa sasa wameanzisha msako mkali wa kumsaka Athumani, ili waweze kumkamata na kumfikisha mbele ya mahakama kujibu tuhuma inayomkabili.

Kwa hisani ya Mo Blog
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa