MFANYABIASHARA ATEKWA,POLISI WAMUOKOA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. POLISI mkoani Singida inashikilia watu watatu, akiwemo mganga wa tiba asilia kutoka Tanga, kwa tuhuma za kumteka nyara mfanyabiashara mkazi wa Manyoni. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alidai utekaji huo ulifanyika Machi 21, mwaka huu saa 9.30 alasiri mjini Manyoni. Wanaoshikiliwa ni Saidi Mgolola (Pesambili) (49) ambaye ni mganga wa tiba za asili, Faraji George (35) ambaye ni mfanyabiashara wa Dodoma na Michael Peter (26), mkazi wa Moshi. Kwa mujibu wa Kamanda, siku ya tukio, watuhumiwa wakiwa kwenye Toyota Prado T.242 CBM, walifika dukani kwa Mathew Dominic (Cheupe) ambaye ni mfanyabiashara, na kujitambulisha kuwa maofisa usalama wa taifa...

Queen Mlozi ashiriki operasheni ya kuondoa mawe makubwa yaliyokuwa yakitumiwa kuteka magari barabara kuu ya Singida-Dodoma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akipasua jiwe kubwa ili liweze kupandishwa kwenye lori kwa lengo kuondolewa kando kando ya barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida. Mawe hayo makubwa kwa kipindi kirefu yametumiwa na watu wanaodhaniwa ni majamabazi watekaji wa malori na kupora mali na fedha. Mkazi wa kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida, Juma akipasua jiwe kubwa lililokuwa likitumiwa na majambazi kwa ajili ya kuteka magari na kisha kupora abiria.   Askari ...

News: Wafanyabiashara watekwa na maafisa usalama feki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake. Na Nathaniel Limu, Singida WAFANYABIASHARA wa Manyoni mjini mume na mke,wametekwa na watu watatu waliojifanya kuwa ni maafisa usalama wa taifa makao makuu jijini Dar-es-salaam. Waathirika wa utekaji huo ni Methew Dominik @ Cheupe (46) na mke wake Selina Methew (42). Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea juzi saa tisa...

Tundu Lissu akabiliwa na changamoto ya michango

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida, Mboya David akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake. Meza ya mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida mashariki linaloshikiliwa na CHADEMA. Kutokana na ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida mashariki kutokuwa na kabati za kutunzia nyaraka imelazimika kutumia viti vya plastiki kutunza nyaraka mbalimbali. Mwalimu Mboya David kaimu mkuu wa shule ya sekondari ya kata Unyahati jimbo la Singida...

Tunamwonea bure Jaji Warioba

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Nchi hii kwa kweli ina visa sijawahi kuviona mahali kwingine katika dunia hii. Ni nchi ya ajabu na sijui ilikuwaje nikaishi humu. Kuna mambo mengi yanayotokea na kunilazimisha baadhi ya nyakati kulaani kwa nini nimekuwa Mtanzania, yaani inachosha sana. Hivi sasa kuna hizi harakati za kutafuta Katiba mpya hapa nchini. Iliundwa tume maalumu ya kutusaidia kupata katiba hiyo. Watu kutoka makundi mbalimbali wakateuliwa, wakiwamo wanasiasa kutoka chama tawala cha CCM na hata vyama vya upinzani. Makundi mengine nayo yakashirikishwa ipasavyo. Baada ya kumaliza kazi...

WANAWAKE WASISITIZWA KUWAKUMBUKA WENZAO WALIOKO MAGEREZANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.   Mtoto Njiti akiwa amebebwa na mama yake. WANAWAKE Mkoani Singida wamehimizwa kujenga tabia ya kuwakumbuka wanawake wenzao waliofungwa na walioko mahabusu gerezani ili waendelee kuaminiwa kuwa bado ni sehemu muhimu ya wanawake mkoani humu. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake kanisa la Free Pentekoste church Tanzania (UWW-FPCT) tawi la Singida mjini, Lessi Jaredi muda mfupi baada ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwa wanawake wanatumikia adhabu jela na wale...

Mama mlemavu wa ngozi ashikiliwa kwa kumuua mwanawe

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela   Polisi mkoani Singida inawashikilia wanawake wawili akiwamo mlemavu wa ngozi (albino), kwa mauaji ya mtoto Daud Richard (2.5), kwa imani za kishirikiana.   Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela (pichani), alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 1:30 asubuhi katika kijiji cha Nkalankala tarafa ya Nduguti, wilaya Mkalama.   Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni bibi wa mtoto huyo, Neema Paulo (35) na mama wa marehemu,...

Wasichana 35 wafukuzwa shule kwa mimba, utoro

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. BODI ya Shule ya Sekondari Munkinya, Kata ya Dung’unyi wilayani Ikungi, Singida imewafukuza shule wanafunzi 35 kwa sababu za utoro, mimba na ukosefu wa nidhamu. Mkuu wa Shule hiyo, Joseph Kilinga, alisema wanafunzi hao walifukuzwa kati ya mwaka 2010 hadi mwaka huu. Alifafanua kwamba katika kipindi hicho jumla ya wanafunzi 21 walifukuzwa shule kwa utoro, wakati utovu wa nidhamu uliwafukuzisha wanafunzi wanne na wengine watatu walifukuzwa kwa mimba.  Chanzo;Tanzania Dai...

NEWS: WAFUNGWA MIAKA 1O JELA KWA KUSABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI WAKATI WA KUTOA MIMBA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Aliyekuwa tabibu msaidizi wa Dispensari ya Tumaini mjini Singida, (wa mbele) Godlisten Raymond (37) na mfanyabiashara wa mbuzi na biashara ya kusaga nafaka (wa tatu mbele) Adamu Shaban Hole (46) mkazi wa kijiji cha Kitandaa tarafa ya Sepuka wilaya ya Ikungi,wakisindikizwa na askari polisi kwenda gerezani kuanza kutumikia adhabu ya kila mmoja kifungo cha miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtoa mimba mwanafunzi na kusababisha kifo chake. Mfanyabiashara wa Mbuzi na kusaga nafaka katika kijiji cha...

KDU wakamata majangili zaidi ya 600

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  KIKOSI cha Kuzuia Ujangili (KDU) Kanda ya Kati, kimefanikiwa kukamata majangili 692 na meno ya tembo 195 katika Operesheni Tokomeza Ujangili iliyofanyika wilayani Manyoni, Singida kuanzia mwaka 2009 hadi 2012. Kaimu Meneja wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Rungwa, Batholomeo Mganga, alisema hayo wakati wa kumkabidhi baiskeli ya miguu mitatu mlemavu, Yohana Pangarasi, mwanakijiji wa Imalampaka, Manyoni. Mganga alisema katika kipindi hicho tembo 168 wenye uzito wa kilo 166...

Chama cha waandishi Wanawake chatoa msaada wa Mizinga 80 ya Nyuki

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Katibu wa chama cha waandishi wanawake (Women in Media Organization - WMO) tawi la mkoa wa Singida, Awila Silla, akitoa taarifa yake ya msaada wa mizinga 80 kwa vikundi vinne vya wafuga nuki wanawake kutoka wilaya ya Singida na Ikungi.     Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa mizinga ya nyuki kwa vikundi vinne vya Wanawake wafuga Nyuki.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi na kulia ni mwenyekiti wa WMO Evarista Lucas.   Mkuu ...

Hatari: Mkulima akamatwa na Bhangi misokoto 888 yenye uzito gramu 44

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela. Na Nathaniel Limu, Singida JESHI la Polisi mkoa wa Singida linamshikilia Mariamu Songeraeli (32) mkulima mkazi wa kijiji cha Nselembwe wilaya ya Iramba kwa tuhuma ya kumiliki madawa ya kulevya aina ya bhangi misokoto 88 yenye uzito wa gramu 44. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema mtuhumiwa Mariamu amekamatwa juzi saa 11.30 jioni nyumbani kwake katika kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui wilaya...

ABIRIA WAKWAMA SINGIDA

ABIRIA waliokuwa wanasafiri  kutoka Dodoma kuelekea  mikoa  ya kanda ziwa,  magharibi  na  nchi jirani,  leo asubuhi wamekwama kwa zaidi ya saa nne  katika eneo la Kijiji cha Kisaki umbali wa Kilomita 10  kabla ya kufika Singida mjini baada ya madereva wa malori kufunga barabara . Zaidi ya malori 300 yaliegeshwa barabarani  kuanzia  saa 12 hadi saa 4 asubuhi, kuzuia  magari mengine yasipite ili kulishinikiza jeshi la polisi kudhibiti uhalifu wa mara kwa mara katika eneo hilo baada ya wenzao wawili kutekwa na majambazi, kujeruhiwa kisha kuporwa  fedha  na mali nyingine. Madereva hao wamesema wamefikia uamuzi wa kufunga barabara ili kuwasilisha hisia zao kwa mamlaka  husika baada ya eneo  hilo na utekaji magari...

Serikali yashauriwa kuajiri Waganga wa Jadi kupunguza uhaba wa watumishi wa Afya

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Kaimu meya mstahiki wa manispaa ya Singida, Hassan Mkata akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Singida kilichofanyika mkoani Singida.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida. Robert Mahili na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida,Hamisi Nguli. Diwani wa kata ya Unyamikumbi,Mosses Ikaku, akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Singida kilichofanyika mjini Singida. Afisa  Ardhi manispaa ya Singida, Angelus John  Camara,akitoa...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa