KIGODA ATAKA TAFITI ZITUMIKE KUTUNGA SERA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda
Watafiti nchini wametakiwa kuwasilisha matokeo ya tafiti zao serikalini, ili zitumike katika kutengeneza sera zinazohusiana na maendeleo ya watu.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uendelezaji wa ujasiriamali  na biashara ndogo na za kati, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Hotuba ya Dk. Kigoda ilisomwa kwa niaba yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Joyce Mapunjo.

Dk. Kigoda, alisema kuna tafiti nyingi zimefanywa na wanataaluma tofauti, lakini hazijaisaidia jamii kwa vile zimehifadhiwa kwenye makabati ndani ya taasisi wanazozifanyia kazi badala ya kuziweka wazi kwa jamii ikiwamo kuziwasilisha serikalini.

Aliwataka watafiti, wajasiriamali, wanataaluma  na wakurugenzi wa mashirika zaidi ya 150 wanaoshiriki mkutano huo wa siku mbili, kufanya majadaliano na tafiti ambazo zitaleta mawazo yaliyo na umuhimu kwa Watanzania.

“Haya mambo ya tafiti yana mambo mengi, sasa na ninyi myaangalie hayo, mkae chini na kutafakari na kuleta mawazo ambayo yatawasaidia Watanzania, kwani mnaweza kufanya tafiti zisiwe na faida kwa mazingira ya Tanzania, lakini yakawa ni mazuri kwa mazingira ya nchi nyingine,” alisema.

Dk. Kigoda, alisema mchango wa biashara ndogo ndogo ni mkubwa na muhimu katika kujenga uchumi wa Taifa na kupunguza umaskini, hivyo serikali itaendelea kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili wajikomboe kiuchumi.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Utawala), Profesa Yunus Mgaya, alisema kila mwaka shule ya biashara ya chuo hicho (UDBS), inaandaa mkutano kama huo, ili kuwakutanisha watafiti kutoka vyuo vikuu mbalimbali pamoja na wajasiriamali.

Alisema lengo la mikutano hiyo ni pamoja na kubadilishana uzoefu na kusaidiana kwenye masuala ya kitaalamu.

Profesa Mgaya, alisema serikali ni lazima iwe na sera za kuwasaidia wajasiriamali, na ndiyo maana wamekuwa wakiishirikisha kwenye mikutano yao kwa kuwa mchango wa wafanyabiashara wadogowadogo ni mkubwa na unatoa ajira kwa watu wengi.
 
SOURCE: NIPASHE

MWANAFUNZI MLEMAVU MIKONO YOTE MIWILI AOMBA MSAADA WA JK

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DSC08466
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Julius Charles (12) ambaye anatumia mguu wa kulia kuandika kutokana na kutokuwa na mikono.Pia anatumia mguu huo kutandika kitanda chake.
DSC08477
DSC08482
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Olivary Kamilly, akimsaidia mwanafunzi Julius Charels Kumvalisha soksi baada ya kutoka darasani.
DSC08497
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wailaya ya Ikungi, Julius Charles, akitandika kitanda chake kwa kutumia mguu wake wa kulia ambao pia anautumia katika kuandika.
DSC08506
Matroni wa mabweni ya kulala wanafunzi walemavu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Modesta Macha, akiwa na wanafunzi wa darasa la sita Julius Charels.
DSC08508
Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Julius Charles,akichukua daftari lake kwa ajili ya kulihifadhi kwenye mfuko wake. Julius anatumia mdomo kwa vile hana mikono.
Na Nathaniel Limu, Ikungi
MWANAFUNZI wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Julius Charles (12) ambaye hana mikono ameiomba serikali imsaidie kupata mtu atakaye mhudumia ili aweze kusoma kwa uhuru zaidi aweze kufikia lengo lake la kusoma hadi chuo kikuu.

Julius amesema amefikia uamuzi huo wa kuomba kupatiwa mtu wa kumhudumia kutokana na kutokuwa na mikono.

Amedai ulemavu huo, umesababisha pamoja na mambo mengine atumie mguu wake wa kulia kuandika na kutandika kitanda.

Julius amefafanua zaidi kwa kusema ulemavu wake huo vile vile, unasababisha ashindwe kuoga,kufua nguo zake na kwamba anapata taabu kubwa wakati wa kujisaidia chooni.
"Kutoa madaftari na kalamu ndani ya mfuko,natumia mdomo wangu.Pia kwa vile sina mikono natumia mdomo kuchukua chakula kutoka kwenye sahani",amesema.

Julius anasema binafsi anamshukuru na kumpongeza rais Kikwete,kwa moyo wake wa kuwajali walemavu wa aina mbalimbali.

"Nina imani kwamba kama ningeonana na Rais Kikwete kwa jinsi anavyowajali walemavu mimi mwenye uchu mkubwa wa kujisomea ataweza kunisaidia kupata mtu wa kunihudumia.Hata hivyo,sikati tamaa kusaidiwa na Rais wetu Kikwete.Akisoma habari hii kwenye Mtandao huu,nina hakika atanisaidia ili ndoto yangu ya kufika chuo kikuu siku moja iweze kuwa kweli",amesema Julius.

Kwa mujibu wa mwalimu wake,Ana Mjema, Julius kwenye mitihani mbalimbali huwa anashika nafasi ya tatu au ya nne.

Amesema mwanafunzi huyo asiye na mikono,kwa kutumia mguu wake ana mwandiko mzuri kuliko wanafunzi wasio na ulemavu.Pia ana kasi katika kuandika.

(Picha zote na Nathaniel Limu).

MO ATAKA MADHEBEBU DINI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI ILI KULETA MAENDELEO ENDELEVU‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DSC_0575
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na waumini wa Msikiti wa kijiji cha Mtamaa wakati wa ziara yake ya siku tatu jimbo kwake.
Na Nathaniel Limu, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gulam Dewji amewahimiza waumini wa madhahebu mbalimbali ya dini kuendelea kushirikiana na serikali ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo endelevu.
Mbunge Dewji maarufu kwa jina la MO,ametoa wito huo hivi karibuni kwa nyakati tofauti wakati akikagua ujenzi wa misikiti na makanisa jimboni kwake.
Amesema madhehebu ya dini mbalimbali yana mchango mkubwa sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo,kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa ujumla.
DSC_0467
Mbunge MO akijumuika na waumini wa Kanisa la FPCT kutoa burudani wakati wa ziara ya MO.
"Mchango wa madhehebu ya dini unasaidia mno kuendeleza amani na utulivu kuanzia ngazi ya kaya,kijiji hadi taifa.Amani na utulivu uliopo hivi sasa ndio unaotusaidia tumwabudu Mungu kwa uhuru na pia kujiletea maendeleo bila vikwazo",amesema.
Dewji amesema ili kuonyesha imani yake kubwa kwa madhehebu ya dini safari hii ameamua kukagua ujenzi wa makanisa na misikiti ya jimboni kwake ili aweze kuyaunga mkono katika ujenzi huo unaoendelea.
"Ninyi ni mashahidi wangu wazuri juu ya maendeleo ya sekta mbalimbali tuliyoyapata jimboni mwetu kwa kushirikiana mimi na ninyi.Baada ya kufanya makubwa kwenye sekta ya elimu,afya,barabara na maji,sasa nimeamua kwa moyo wangu wote kuboresha ustawi wa madhehebu ya dini",amesema.
Akifafanua zaidi, amesema kupitia kwa katibu mkuu wa CCM taifa,anatarajia kukabidhi misaada ya mabati na mifuko ya saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi 127 milioni kwa misikiti 51 na makanisa 30.

MH. MOHAMMED G.DEWJI (MO) AMWAGA MSAADA WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 127 KWENYE TAASISI ZA DINI ZAIDI 80 JIMBONI KWAKE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
DSC_0025
Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya ndoa.
DSC_0029
Sheikh wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.
DSC_0133
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo, ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi kutoa Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
DSC_0171
MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.
DSC_0237
Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.
DSC_0262
Baadhi ya wapiga kura wa kijiji cha Mangwanjuki wakipeana mikono ya Kheri na Mbunge wao.
DSC_0287
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Mwankonko darajani wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) wakati alipoendelea na zoezi la kutembelea nyumba za kuabudu zilizopo jimboni kwake.
DSC_0314
Jengo la wa Mwankonko darajani likiwa kwenye hatua Lenta, ambapo baada ya Mbunge kuona hatua hiyo ya nguvu za wananchi aliahidi Bati 50 na Mifuko ya Saruji 50.
DSC_0713
Mheshimiwa Mohammed Dewji na baaadhi ya viongozi wa Msikiti wa kijiji cha Kisasida.
DSC_0729
Mbunge MO akizungumza na waumini wa Msikiti wa Kisasida, ambapo ameahidi kutoa msaada wa Mabati 100 na Mbao 100 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Msikiti huo.
DSC_0738
MNEC wa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala akitoa hamasa kwa wakazi wa Kisasida kushiriki Mkutano wa hadhara ambao umeitishwa kwa ajili ya Katibu Mkuu CCM Taifa, Abdulrahman Kinana wa kuongea na wakazi wa jimbo la Singida Mjini utakaofanyika viwanja vya People’s Club.
DSC_0750
Mheshimiwa Mohammed Dewji akielekea kukagua ujenzi wa Msikiti wa Minga mjini Singida.
DSC_0336
Watoto wa Madrasa ya Msikiti wa Mwankoko Darajani wakimpokea Mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati alipotembelea ujenzi wa Msikiti huo.
DSC_0343
Mheshimiwa Mohammed Dewji akifurahia jumbe zilizoandikwa na watoto wa Madrasa ya Mskiti wa Mwankoko Darajani.
Kwa picha zaidi bofya hapa

KINANA AWASILI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ndugu Lazaro Nyalandu katika kijiji cha Kaskazi mkoani Singida,Katibu Mkuu atakuwa kwenye ziara ya siku nane mkoani Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidiana na mafundi kupandish bati wakati wa ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Mgando,Singida
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa CCM mkoa wa Singida na Kundi la akina mama wajasiriamali wa Itagata kuelekea kwenye mkutano wa hadhara  baada ya kufungua shina la akina mama hao wa Itagata,Singida.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa bwawa la maji la Itagata,Singida.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Itigi mkoani Singida .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Itigi na kuwaambia  CCM ipo imara na kuwaambia wananchi hao muungano  wa vyama vya siasa unaofahamika  kama UKAWA ndio utahitimisha maisha ya baadhi ya vyama vya siasa nchini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma barua ya wakazi wa Tura ambao wanahitaji kujengewa kivuko kwenye reli ili kuwasaidia kwenda kuchota maji bila matatizo kwani kwa sasa wanapata tabu,Katibu Mkuu alisimama Tura kuwasalimu wananchi na kisha kuendelea na safari kuelekea Singida.

AJALI YAUA WATANO NA KUJERUHI 16 MLIMA SENKENKE MKOANI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace eneo la Mlima Sekenke, wilayani Iramba kwenye Barabara Kuu ya Singida -Mwanza. 

Mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Dk Antony Mbulu, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati abiria hao wakienda kwenye sherehe ya Maulid kijiji jirani cha Shelui.
Dk Mbulu aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva Athuman Adam (34) na Ally Wambura (36), wakazi wa Igunga na Amin Salim (45) mkazi wa mjini Singida. Alisema miili ya watu wawili haijatambuliwa.
Kwa mujibu wa Dk Mbulu, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T547 ASP kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi.

Alisema kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo, wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi huku hali zao zikielezwa kuwa mbaya.
Baadhi ya majeruhi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
Walidai kuwa ajali ilitokea wakati dereva huyo akipita malori kwa kasi, ndipo akagonga kingo za barabara na kupasua tairi kabla ya kuingia msituni na kupinduka mara nne.


Basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 likitoka mjini Singida kwenda Shelui.

Waandishi wa habari wapewa changamoto ya ubunifu, kujituma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na Nathaniel Limu, Singida
WAANDISHI wa Habari mkoani Singida, wamehimizwa kuondokana na uandishi habari wa mazoea na badala yake wabadilike na kuwa wabunifu ili kazi yao iweze kukidhi viwango vya wakati uliopo.
Changamoto hiyo imetolewa hivi karibuni na mwandishi wa habari mkongwe, Eda Sanga wakati akizungmza kwenye semina ya Uhabarisho wa Mfuko wa Habari Tanzania (Tanzania Media Fund TMF) kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida.
Amesema waandishi wa habari ule wa business as usual, haufai umepitwa na wakati unadumaza maendeleo ya mhusika.
amesema uandishi wa habari kwa sasa umetakiwa mwandishi wa habari ujitume, uwe mbunifu, ufanye uchunguzi wa kina ili ukiandika habari watu wakupongeze au wakusifu.
pics 3“Ninyi mnapaswa katika kutekeleza majukumu yenu muiangalie Singida kwa upana wake. Ni kero gani zinawasibu wananchi. Nini kifanyike ii kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kero hizo”
  Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida,wakifuatilia mada   zilizokuwa zinatolewa na maafisa kutoka Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) juu ya kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na mfuko huo.Picha na Nathaniel Limu.
pics 1Afisa kutoka Mfuko wa Waandishi wa Habari Tanzania (TMF) Alex Kanyambo akitoa mada yake juu ya umuhimu wa vilabu vya waandishi wa habari kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na TMF.Wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa TMF,Japhet Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,Seif Takaza.
Kwa hali hiyo, aliwataka kujitathimini juu ya utendaji wao wa kila siku na wahakikishe habari zao zisiwe na upande moja mbali ziwe ‘balanced’.
pics2Mwandishi wa habari mkongwe nchini,Eda Sanga akizungumza kwenye semina ya uhabarisho juu ya shughuli za Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) iliyohudhuriwa na waandishi wa habari mkoa wa Singida.
Awali Afisa Habari wa TMF makao makuu,Japhet Sanga amewahimiza waandishi wa habari nchini kujenga utamaduni wa kuomba uwezeshaji wa fedha kutoka TMF ili pamoja na mambo mengine kuongeza uzoefu zaidi katika kutekeleza majukumu yao.
Akifafanua, amesema TMF inatoa ruzuku ya fedha kwa ajili ya waandishi wa habari kuandika habari za uchunguzi ambazo zinaibua mambo mengi mapya na hasa kero zinazowakabili wananchi wakiwemo wa vijijini.
“TMF tunaamini kwamba kwa vyo vyote habari za uchuguzi zitamwezesha mwandishi husika kujifunza mambo mapya kwa hiyo atakuwa amepanua wigo wa ufahamu wa mambo mengi”.,amesema.

'NILIANZA KAZI NIKAMKUTA AMELAZWA ,SASA NAKARIBIA KUSTAFU NITAMWACHA'

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Muuguzi wa Wodi Namba Nne katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, Belta Lyamboko amesema alipoanza kazi katika hospitali hiyo mwanzoni mwa mwaka 1981, alimkuta Mzee Abdi Lanjuu (75) na sasa anajiandaa kustaafu akiamini atamwacha mzee huyo hospitalini.
Mzee Lanjuu amelazwa hospitalini hapo kwa miaka 43 sasa baada ya kupata ajali ya lori mwaka 1971, alipokuwa mtumishi wa iliyokuwa Mamlaka ya Pamba Tanzania (TCA), Mkoa wa Mwanza.
Kuishi kwake hospitalini hapo kwa miaka mingi, kumechangiwa na kutokuwa na ndugu wala rafiki wa kumhudumia. “Wakati ninaanza kazi nikiwa kijana, Mzee Abdi alikuwa na nguvu na alikuwa akitembelea kiti cha magurudumu, lakini katika miaka mitatu au zaidi hali yake imekuwa mbaya na hawezi kutembea hata kwa kutumia kiti chake cha magurudumu. Kila kitu pamoja na kula anafanya akiwa amelala kitandani na anasaidiwa na wauguzi... tumeshamzoea na ametuzoea na sasa tunaishi naye kama ndugu,” alisema.
Alisema kuwa tangu aanze kumwona mzee huyo hospitalini hapo, hakuwahi kuwaona ndugu wala rafiki wanaokuja kumtembelea au kumjulia hali.
“Kutokana na hali hiyo na kukaa naye kwa miaka 43 sasa, kila mmoja anamwona ni ndugu, sasa utamfanya nini na yuko hapa...tunaishi naye, tunampatia misaada midogomidogo ya kumwezesha kupata mlo, kinachopatikana tunampatia na tunaendelea kumsaidia, hatutachoka,” alisema.
Chanzo:Mwananchi

DEREVA AFARIKI AKIFNYA MAPENZI 'GESTI'

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Juma Juma (52), amefariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa na mwanamke ambaye imedaiwa ni mhudumu wa baa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema tukio hilo lilitokea  Mei 3, saa 4:00 usiku chumba kwenye Na. S.2 cha nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life New mjini Kiomboi.
Alisema saa 6:00 usiku siku ya tukio hilo, dereva huyo alimuaga mpangaji wake kuwa anatoka mara moja na hangechelewa kurudi nyumbani kwa hiyo asifunge mlango wa mbele ya nyumba.
Alisema kuwa saa mbili baadaye, dereva huyo alionekana akiwa baa iliyoko kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni ambayo iko mita 50 kutoka nyumbani kwake.
“Muda huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo aitwaye Agness Mayo (32) anayesadikiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi,” alisema.
Kamwela alisema mhudumu huyo wa baa alitoweka Mei 4, mwaka huu baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na kutorokea kusikojulika.
Hata hivyo, ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa chumba cha kulala wahudumu wenzake.
Kamanda huyo alisema kuwa tangu siku Mei 3, chumba alicholala Juma hakikufunguliwa hadi Mei 5 mwaka huu wakati mwili wa dereva huyo ulipokutwa ukiwa umeharibika.
“Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta mhudumu aliyetoroka ili ahojiwe na kisha kufikishwa mahakamani endapo atabainika kuhusika na tukio,” alisema kamanda Kamwela.
Chanzo:Mwananchi

AJABU NA KWELI,TUKIO KATIKA PICHA NA HABARI KAMILI: Mzee aishi wodini kwa miaka 45 tangu Januari mosi mwaka 1971

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC07576
Mzee Abdi Nkhambi Lanjui (75) akiwa wodi namba nne katika hospitali ya mkoa mjini Singida. Mzee Lanjui mzaliwa wa kijiji cha Mhintiri tarafa ya Ihanja, aliyekuwa dereva wa kampuni ya mamlaka ya Pamba Mwanza, alipata ajali katikati ya mwaka 1968 na kulazwa katika hospitali ya Sekoture Mwanza na baadaye mwishoni mwa mwaka 1970,alihamishiwa hospitali ya mkoa wa Singida, ambako anaishi hadi sasa. Ajali hiyo ilisababisha kukatika mawasiliano kati ya kuanzia kiunoni na kushuka chini ambako kumepooza na sasa kuna vidonda na sehemu ya mwili juu ya kiuno, bado inafanya kazi.(Picha na  Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MZEE Abdi Nkhambi Lanjui (75) ambaye ameishi wodini kwa miaka 45 sasa ameiomba serikali,Asasi na jamii kwa ujumla kumsaidia huduma ya chakula kwa madai kwamba hana ndugu wa kumsaidia huduma hiyo.
Akizungumza na MOblog hivi karibuni, Mzee Abdi ambaye kwa sasa hawezi kabisa kunyanyuka kitandani amesema kuwa kwa miaka mingi uongozi wa hospitali ya mkoa umemhudumia vizuri chakula cha kutosha.
 Akifafanua amesema baada ya hospitali hiyo kusitisha huduma ya chakula kwa wagonjwa amekuwa omba omba na maisha yake yamebaki ya mlo moja kwa siku.
 “Kwa vile siwezi kunyanyuka kitandani na sina ndugu ye yote nimekuwa nikiwaomba msaada manesi na watumishi wengine wa hospitani hapa na nashukuru sana hawaniangushi wamekuwa wakinisaidia bila kuchoka na wananiwezesha kupata angalau mlo wa siku moja”,amesema.
DSC07582
Mzee Abdi pia ametumia fursa hiyo kuomba msaada wa fedha na msindikizaji kwa ajili ya kwenda hospitali ya KCMC Moshi mkoa wa Kilimanjaro ili akapatiwe huduma ya matibabu.
 “Sababu ya mimi kugeuza wodi kuwa makazi yangu ya kudumu ni kutokana na ajali iliyosababisha kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo za miguuni,kupooza Kwa sababu hivi sasa sinyanyuki kitandani kumepelekea nipate vidoda kuanzia makalioni hadi kwenye miguu kwa ujumla kwa sasa naishi maisha magumu mno”amesema Mzee Abdi.
Mzee Abdi amelazwa wodi namba nne katika hospitali ya mkoa mjini hapa toka januari mosi mwaka 1971.
Awali alilazwa katika hospitali ya Sekoture ya jijini Mwanza kuanzia mwaka 1969 baada ya kupata ajali ya lori alilokuwa akiliendesha kupasuka tairi la mbele.
DSC07584
Amesema akiwa hospitali ya Sekoture mwishoni mwa mwaka 1970 hali yake ilibadilika na kuwa mbaya na ndipo alipomwomba mwajiri wake mamlaka ya pamba imrudishe nyumbani katika kijiji cha Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi ili akasubiri kifo chake.
Hata hivyo,amesema uongozi wa mamlaka ya pamba ulikataa kumpeleka kijijini kwao na badala yake walimkabidhi katika hospitali ya mkoa wa Singida mapema mwaka 1971.
Mzee Abdi amesema aliondoka nyumbani kwao Mhintiri mwaka 1962 na kwenda Mwanza mjini kusaka maisha bora alijifunza udereva na kisha kufanikiwa kuajiriwa na mamalaka ya pamba mwaka 1968.Wakati akiondoka kwao alimwacha baba,mama na kaka yake mkubwa.
Toka alazwe hospitalini,wazazi wake na ndugu yake pekee walikuwa tayari wamefariki dunia kwao walizaliwa watoto wawili tu wa kiume.

SUMRY YATOA UBANI WA SH.5.5M AJALI SINGIDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

“Tangu kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu

Uongozi wa Kampuni ya Mabasi ya Sumry ya Sumbawanga, Rukwa umetoa ubani wa Sh5.5 milioni kwa familia za ndugu na jamaa waliofariki dunia kutokana na ajali ya moja ya mabasi yake iliyotokea Aprili 28 katika Kijiji cha Utaho, Wilaya ya Ikungi, Singida.
Katika ajali hiyo, watu 19 wakiwamo polisi wanne, walifariki papohapo baada ya kugongwa na basi hilo lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori na mwendesha baiskeli ambaye alipoteza maisha katika eneo hilo baada ya kugongwa na lori hilo. Wakazi hao waliogongwa walikuwa wamekusanyika kushuhudia ajali hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hipoliti Daniel Kholani alisema rambirambi hiyo ilikabidhiwa kwa Serikali ya Kijiji na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone ambaye naye alichangia Sh100,000.
Kholani alisema pia Mbunge wa Singida Magharibi, Mohamed Missanga ametoa Sh600,000 na wakazi wa Tarafa ya Ihanja waishio jijini Dar es Salaam pia wamechanga Sh600,000.
“Tangu kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu.”
Kholani alisema wakazi wa kijiji hicho, Mussa Mohammed, Suku Abdallah na Ayubu Ramadhani bado wamelazwa hospitalini wakiendelea kutibiwa majeraha waliyoyapata kwenye ajali ya basi hilo ambalo bado lipo Kituo cha Polisi Ikungi.Uongozi wa Kampuni ya Mabasi ya Sumry ya Sumbawanga, Rukwa umetoa ubani wa Sh5.5 milioni kwa familia za ndugu na jamaa waliofariki dunia kutokana na ajali ya moja ya mabasi yake iliyotokea Aprili 28 katika Kijiji cha Utaho, Wilaya ya Ikungi, Singida.
Katika ajali hiyo, watu 19 wakiwamo polisi wanne, walifariki papohapo baada ya kugongwa na basi hilo lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam.
Ajali hiyo ilitokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori na mwendesha baiskeli ambaye alipoteza maisha katika eneo hilo baada ya kugongwa na lori hilo. Wakazi hao waliogongwa walikuwa wamekusanyika kushuhudia ajali hiyo.
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hipoliti Daniel Kholani alisema rambirambi hiyo ilikabidhiwa kwa Serikali ya Kijiji na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone ambaye naye alichangia Sh100,000.
Kholani alisema pia Mbunge wa Singida Magharibi, Mohamed Missanga ametoa Sh600,000 na wakazi wa Tarafa ya Ihanja waishio jijini Dar es Salaam pia wamechanga Sh600,000.
“Tangu kutokea kwa ajali hiyo kijiji kimeendelea kupata idadi kubwa ya wageni kutoka sehemu mbalimbali kuja kutoa pole kwa wafiwa. Tunatarajia kufanya sala maalumu kwenye eneo la tukio kesho (leo), kuwaombea ndugu zetu.”
Kholani alisema wakazi wa kijiji hicho, Mussa Mohammed, Suku Abdallah na Ayubu Ramadhani bado wamelazwa hospitalini wakiendelea kutibiwa majeraha waliyoyapata kwenye ajali ya basi hilo ambalo bado lipo Kituo cha Polisi Ikungi.
Chanzo:Mwananchi

TANKI MAFUTA LALIPUKA NA KUSABABISHA ADHA KUBWA KWA WASAFIRI MAENEO YA SHELUI SINGIDA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
7Baadhi ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B. Clarke Haulege Construction, Tanki hilo ni mali ya Bw. Bundala Kapela wa Igunga ni namba T634 BCZ lenye vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita 40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto, Jambo lililomfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ilu kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea, Katika tukio hilo lililosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na msururu wa magari kushindwa kupita katika eneo hilo kutokana na moto mkubwa uliochanganyika na moshi kutishia usalama wa watumiaji wengine, hata hivyo baada ya moto kupungua kiasi askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea na safari hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo, Angalia matukio zaidi ya picha hapo chini. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SHELUI-SINGIDA) 5 4 3 2 111Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka. 10Wananchi na wasafiri mbalimbali wakitoka kuangalia tukio hilo. 8Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawana usalama unaimarishwa katika eneo hilo.

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KUMWAGA NEEMA SINGIDA KWA KUJENGA NYUMBA 200 ZA KUKOPESHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC08020
Mkuu wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF)  mkoa wa Singida, Bw. Saidi Majimoto, akihamasisha wanafunzi wa ualimu kujinga na mfuko wa PSPF ili kujihakikishia kupata mafao ya kukidhi mahitaji.Kushoto ni afisa wa PSPF, Andrew Mtima.
DSC08012
Baadhi ya wanafunzi wa ualimu chuo cha Lake Hill mjini Singida,wakimsikiliza mkuu wa mfuko wa pensheni kwa watumisi wa umma (PSPF), Saidi Majimoto (hayupo kwenye picha)akiwahamasisha kujiunga na mfuko huo ili kufaidika na mafao lukuki.
DSC08013
Bango la PSPF.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MFUKO wa Pensheni kwa watumishi wa Umma (PSPF) unakusudia kujenga nyumba 200 za gharama nafuu mkoani Singida kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wake.
 Mkuu wa PSPF mkoani Singida, Said Majimoto alieleza hayo hivi karibuni wakati akitambulisha Mfuko huo kwa wanachuo wa Chuo cha Ualimu Lake mjini hapa.
 Majimoto amesema kuwa mfuko huo umechukua hatua hiyo ili kuwawezesha wanachama wake kuishi mahali pazuri pasipo na usumbufu na kwa kwa bei nafuu kabisa.
Amesema kuwa kwa hivi sasa michoro ya viwanja hivyo, ambavyo vipo eneo la Mandewa iko tayari na kwamba ujenzi wa nyumba hizo unatarajiwa kuanza wakati wowote.
 Majimoto alifafanua kuwa PSPF hutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama waliochangia miaka mitano na kuendelea ambapo hulipa kidogo kidogo kupitia mishahara yao kwa muda wa miaka hadi 25. “Mwanachama huanza kuishi katika nyumba yake mara tu anapoanza makato ya mkopo husika” amesema.
Aidha, alidokeza kuwa PSPF hutoa mikopo ya fedha  kwa kiwango cha hadi nusu ya mafao ya mwanachama aliyebakiza miaka mitano kustaafu, kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na ununuzi wa nyumba mahali popote anapoamua mwanachama huyo.
 Mhasibu wa mfuko huo kutoka Makao Makuu, Andrew Msina amesema kuwa hadi sasa mfuko huo una wanachama 400,000, kati ya idadi hiyo asilimia 97 ya walimu walio kwenye ajira ni wanachama. Alisema kuwa wingi huo wa wanachama unatokana na ukweli kwamba PSPF ina aina ya kikokotoo bora zaidi kuliko mfuko mwingine wowote wa jamii nchini.
Msina pia amesema kuwa hadi Juni 2013 PSPF ilikuwa imelipa mafao ya sh. bilioni 543.7 kwa wastaafu mbalimbali nchini huku Mfuko huo ukiwa unajivunia thamani ya mafao ya sh. trilioni 1.25 kibindoni.

TAASISI YA MKAPA YAKABIDHI NYUMBA 30

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akikabidhiwa kibuyu na akina mama wa kijiji cha Senenemfuru, Singida vijijini, kikiwa na maana ya upendo, baada ya kukabidhi nyumba, kati ya 30 zilizojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa halmashauri tano za mkoa wa Singida.
 
Rais  mstaafu awamu ya tatu, Benjamin  Mkapa, kupitia taasisi yake ‘Benjamin William Mkapa HIV/AIDS’ (BMAF), amekabidhi nyumba 30 zilizojengwa kwenye zahanati 13 na vituo vya afya viwili kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 1. 9 katika Halmashauri tano za wilaya mkoani Singida.
Akikabidhi sehemu ya nyumba hizo kwenye hafla iliyofanyika kijiji cha Senenemfuru Singida vijijini, Mkapa alishukuru wafadhili waliowezesha kazi hiyo, ukiwamo Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria (Global fund) kwa kuonyesha imani kwa serikali ya Tanzania.

“Binafsi ninafarijika kufahamu kwamba wananchi wanaohudumiwa na zahanati 15 ambazo nyumba hizi zimejengwa, wataendelea kufaidika na huduma bora za afya kutoka vituo hivyo kwa sababu watoa huduma wameboreshewa mazingira ya kazi zao,” alisema Mkapa.

Nyumba hizo zimejengwa katika zahanati ya Misughaa na Mangonyi (Ikungi), Mkenge, Mpambaa na Senenemfuru (Singida), Ulemo Uwanza na kituo cha afya Ndago (Iramba), Kinyambuli na Dominiki (Mkalama). Pia kituo cha afya Itigi, Idodyandole, Heka, Mpola na Chibumagwa (Manyoni).

Mkapa alizihimiza halmashauri za wilaya husika kutunza vyema nyumba hizo na kutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa na alizitaka kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya matengenezo ya mara kwa mara ili zidumu, kuendelea kuwa madhubuti na kuvutia zaidi.

“Hata hivyo, ili kuwa na huduma ya afya bora zaidi na kamilifu, ni lazima kuwapo na zahanati yenye dawa, vifaa vya kutolea huduma na vipimo na uwapo wa wataalamu wa kutosha, wekeni mkakati kuhakikisha hayo yote yanazingatiwa na kutekelezwa,” alisisitiza Mkapa.

Mwakilishi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Catherine Joachim, aliishukuru taasisi hiyo na kusema kupitia mradi huo kwa mwaka wa pili sasa utahusisha ujenzi wa nyumba 220 za watumishi wa afya kwa mikoa ya Arusha, Ruvuma, Manyara, Pwani na Singida.

Aidha, afisa mtendaji Mkuu wa BMAF, Dk. Ellen Mkondya-Senkoro, alisema BMAF mkoani Singida imekuwa ikichangia shughuli mbalimbali ikiwamo kuimarisha huduma za Ukimwi, afya ya uzazi na masuala ya watumishi wa afya tangu mwaka 2006.
SOURCE: NIPASHE
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa