Home » » MFANYABIASHARA ATEKWA,POLISI WAMUOKOA

MFANYABIASHARA ATEKWA,POLISI WAMUOKOA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


POLISI mkoani Singida inashikilia watu watatu, akiwemo mganga wa tiba asilia kutoka Tanga, kwa tuhuma za kumteka nyara mfanyabiashara mkazi wa Manyoni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alidai utekaji huo ulifanyika Machi 21, mwaka huu saa 9.30 alasiri mjini Manyoni.
Wanaoshikiliwa ni Saidi Mgolola (Pesambili) (49) ambaye ni mganga wa tiba za asili, Faraji George (35) ambaye ni mfanyabiashara wa Dodoma na Michael Peter (26), mkazi wa Moshi.
Kwa mujibu wa Kamanda, siku ya tukio, watuhumiwa wakiwa kwenye Toyota Prado T.242 CBM, walifika dukani kwa Mathew Dominic (Cheupe) ambaye ni mfanyabiashara, na kujitambulisha kuwa maofisa usalama wa taifa kutoka makao makuu Dar es Salaam.
"Walimtaka aongozane nao hadi kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, mjini Singida kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Alikubali kwa sharti kwamba aondoke na mkewe, Selina Mathew," alisema Kamanda.
Ilidaiwa badala ya kuelekea barabara ya Singida, walielekea Dodoma lakini kutokana na polisi kupata taarifa mapema, walikamatwa Bahi kwenye kizuizi cha barabarani.
Alisema chanzo cha utekaji huo kinadaiwa kuwania mali ya mfanyabiashara huyo.
Chanzo:Habari Leo 

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa