Nathaniel Limu, Singida
Wataalam wa kilimo kwenye maeneo ambayo ukame umekithiri hapa nchini, wameshauriwa kuunda mtandao wa mawasiliano, utakaosaidia kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na athari zinazosababishwa na ukame.
Changamoto hiyo imetolewa juzi na katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan wakati akifungua semina ya siku tatu iliyohusu kilimo bora cha mtama iliyohuduriwa na wataalamu 47 kutoka wilaya nane za hapa nchini.
Alisema hivi sasa ukame unaosababishwa na uhaba wa mvua, unasababisha pamoja na mambo mengine, uhaba mkubwa wa mavuno ya mazoa ya chakula.
Akifafanua, Liana alisema uhaba huo wa mavuno ya chakula unasababisha baadhi ya maeneo kuwa na njaa kali na hivyo wakazi wake, kushindwa kujiletea maendeleo endelevu.
Aidha, Katibu tawala huyo, amewataka wananchi waishio kwenye maeneo kame, kuacha tabia ya kuchagua vyakula.
Awali ofisa mwandamizi wa shirika lisilo la kiserikali la International Crops Research Institute for the Semiarid Tropics (ICRISAT), lenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Dk. Mary Mgonja, alisema shirika lao limejikita kaitka kuhimiza wananchi kujenga utamaduni wa kulima mazoa yanayostahimili ukame likiwemo zao la mtama, kwa madai kuwa mtama ni zao la chakula na biashara.
“Zao la mtama ni muhimu katika maeneo yanayokabiliwa na ukame na pia sehemu ambazo udongo una rutuba ya wastani. Utafiti wa zao hili umeweza kutoa kenlojia mbali mbali ambazo zinaweza kutumiwa ili kuongeza tija katika uzalishaji”,alisema.
Dk.Mary alisenma kuwa shirika la ICRISAT limepewa msaada wa zaidi ya dola za kimerikani milioni mbili kwa ajili ya kugharamia na kuratibu mradi wa kuhima kilimo bora cha mtama ambao amedai kuwa licha ya kuwa ni chakula bora,kwa sasa lina soko la uhakika.
Alisema wilaya ya Same,Mwanga,Moshi,Kongwa,Singida vijijini,Iramba,Serengeti na Kondoa,kila moja imepatiwa shilingi milioni kumi kwa ajili ya kugharamia mafunzo kwa wakulima na wataalam wa kilo katika hatua ya kwanza ya mradi.
Chanzo: Mo Blog
0 comments:
Post a Comment