MKUTANO MKUU WA TATU WA PSPF WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizindua huduma mpya ya PSPF Pamoja nawe na PSPF call centre, itolewayo na mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kufungua Mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo Feb 26.2014.  Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, kulia kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George Yembesi, Mkurugenzi Mkuu PSPF, Adam Mayingu na Katibu Mkuu MPAIC,...

Ajali Basi la Bunda Lagongana na Treni,watu wanne wafariki dunia

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.    Basi la Bunda Express lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi hii limegongana na Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida.  Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka eneo la tukiokinasema kuwa watu wanne wamefariki dunia na kadhaa kujeruhiwa. Majeruhi Tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni...

TANGASIS WASUSIA FIDIA KIDUCHU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  WAKAZI wa Mwambani, Kata ya Tangasisi, wilayani Tanga wameelezea kutoridhishwa na fidia waliyolipwa ili kupisha ujenzi wa reli kwenye Bandari mpya ya Mwambani. Wakazi hao zaidi ya 200 wanaoishi kandokando ya bahari wamelipwa sh 3,400 kwa mita moja ya mraba wakati viwango vya jiji hilo kwa sasa ni sh 7,000 kwa ukubwa huo kitu kinachowafanya wadai fidia zaidi. Kwa sababu hiyo wamemuomba Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, kuingilia kati suala hilo kwa kuwa thamani ya pesa wanayolipwa hailingani...

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU Mfuko wa Pensheni wa  PSPF unatangaza kwamba kutakuwa na Mkutano Mkuu wa tatu wa wadau utakaofanyika tarehe 26 na 27  Februari 2014 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo barabara ya Shaban Robert  jijini Dar es salaam. Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabili Mfuko na sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla. “PSPF - TULIZO LA WASTAAFU” Mkurugenzi Mkuu Mfuko...

DC Singida awataka Madiwani na watendaji wa kata hadi Mei 30 Ujenzi wa Maabara uwe umekamilika.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.   Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mwashinga Mlozi, akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida.Pamoja na mambo mengine, aliagiza kwamba Diwani na mtendaji wake wa kata wasipomaliza ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara kabla ya Mei 30 mwaka huu, atawachukulia hatua kali ya kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani. Wa pili kulia (aliyeketi),ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Singida,Illuminata Mwenda na anayefuata ni mwenyekiti wa halmashauri ya Singida.MKUU wa wilaya ya Singida,Queen...

Ashikiliwa kwa nyara za Serikali

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  Polisi Mkoa wa Singida, wanamshikilia Jafari Hamisi (23),Mkazi wa Ukombozi mjini Singida,kwa tuhuma ya kumilki kinyume cha sheria vipande 16 vya meno ya ndovu vyenye thamani ya zaidi ya Sh17milioni. Meno hayo yamekamatwa ikiwa ni siku nne toka meno mengine vipande 21 vyenye thamani ya zaidi ya Sh43 milioni,kukamatwa kwenye eneo lile lile la kizuizi cha mazao kilichopo katika Kijiji cha Ukimbu kata ya Mgandu Wilaya ya Manyoni. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.SSP.Cordula Lyimo,alisema meno hayo yamekamatwa Feb 16 mwaka huu saa tano usiku katika kizuizi cha ...

Akamatwa na vipande 21 vya meno ya tembo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  JESHI la Polisi limemkamata mtu mmoja  mkazi wa Mwamagembe, Itigi wilayani Manyoni, Singida, George James (30)  na vipande 21 vya meno  ya tembo akiwa njiani kuvisafirisha. Kamanda wa Polisi mkoani humo (SACP) Geofrey Kamwela, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata kijana huyo baada ya kuweka mtego wakati wakiwa ndani ya gari. Alilitaja gari hilo kuwa ni Toyota Hiace lenye namba za usajili T 797 CQL...

BREAKING NEWS TUKIO KATIKA PICHA: LORI LA MAFUTA LADONDOKA MDA HUU MLIMA SEKENKE LALIPUKA NA KUUWA WATU WA NNE HAPO HAPO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.   Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua  Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii  Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii  Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa  Hii ni njia ya mlima sekenke  Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwam kwenye Lori hiloo   Moto ukimalizikia kwa mbaliii kama inavyoonekana Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida...

JESHI LA POLISI LAKAMATA MENO YA NDOVU YENYE THAMANI SHILINGI MILIONI 17 SINGIDA‏

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SSP.Cordula Lyimo, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo juu ya kukamtwa kwa meno ya Tembo vipande 16 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 17 milioni.Vipande hivyo vimekamatwa februari 16 mwaka huu saa tano usiku kwenye kizuizi cha mazao cha kijiji cha Ukimbu wilaya ya Manyoni. Siku nne zilizopita,vipande vingine 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya shilingi 43 milioni,vilikamatwa eneo hilo hilo.(Picha na Nathaniel Limu). Na Nathaniel Limu, Singida JESHI la Polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata vipande 16 vya meno ya ndovu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17. Meno hayo yamekamatwa...

Mt. Gaspari yatibu wagonjwa 53,000

ZAIDI ya wagonjwa 53,000 walipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspari iliyopo katika mji mdogo wa Itigi, wilayani Manyoni, Singida kwa kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka jana. Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Padre Seraphine Lesiriam, alisema hayo kwenye risala aliyosoma kwa mgeni rasmi Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo wakati wa ufunguzi wa kliniki ya upasuaji wa watoto hospitalini hapo. Padre Seraphine alifafanua kwamba katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2012 watoto waliohitaji huduma za upasuaji hususani wa moyo hupelekwa...

Halmashauri ya Manispaa ya Singida yapongezwa kwa kujenga daraja

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,(wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka mkandarasi wa daraja la Mwankoko manispaa ya Singida,Rogers Mchau(anayenyoosha mkono) juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja kijiji cha Mwankoko. Dk.Kone alilikagua daraja hilo baada ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, kulalamika kwamba fedha zinazotumika katika ujenzi huo ni nyingi hazifanani na daraja lenyewe. Baada ya kulikagua,alikiri kuwa daraja hilo lina thamani na fedha zilizotumika na kwamba bado kuna zaidi ya shilingi 192 milioni zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo. Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone,akikagua ujenzi wa daraja...

MIFUKO YA BIMA YA AFYA (NHIF) NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) SINGIDA YAHIMIZWA KUWA MAKINI KWA MADAI YA KUGHUSHI‏

Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki, akifungua kikao cha waratibu wa mfuko wa Taifa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambacho kilitumika kukumbushana juu ya utoaji huduma bora kwa wananchama.Kulia ni afisa matekelezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya Shekifu na kushoto ni Edwin Mwangajilo afisa udhibiti ubora NHIF.(Picha na Nathaniel Limu). Afisa matekelezo na uratibu wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Singida, Isaya Shekifu akitoa mada yake kwenye kikao cha wataribu wa mfuko wa NHIF na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoa wa Singida.Kikoa hicho kililenga kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi,ili...

Diwani kortini kwa lugha chafu

 DIWANI wa Unyambwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Shabani Salumu (CCM), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Singida, akikabiliwa na tuhuma za kuwatolea lugha ya matusi maofisa wa polisi ikiwemo kudai ni ‘mizigo’. Mbele ya Hakimu Aisha Mwetindwa, Mwendesha Mashitaka, Chemu Mussa, alidai  kuwa Januari 12, mwaka huu, saa 1.30 asubuhi katika Kijiji cha Ijanuka, Kata ya Unyambwa,  mshitakiwa aliwatolea lugha ya matusi maofisa wa polisi kitendo kilichoelekea kusababisha kutoweka au kuvunjika kwa amani. Alidai tukio hilo lilitokea wakati maofisa hao wakiwa kazini kwenye eneo ambalo wananchi wa Kata ya Unyambwa walichoma moto basi la Kampuni ya Mtei. Mshitakiwa alikana tuhuma hizo na yupo nje kwa dhamana....

WAKATI MKUTANO WA KUPINGA UJANGILI DUNIANI KOTE: GEORGE JAMES AKAMATWA NA MENO 21 YA TEMBO YENYE THAMANI YA TSH MILIONI 43, SINGIDA

JESHI la polisi mkoani Singida limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43.  Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe  wilayani Manyoni  zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida.  Mtu mmoja  George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno  hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria.  Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata  ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL. Kamanda...

Tanesco kutumia shilingi 48 bilioni kusambaza Umeme Vijijini Singida.

Meneja wa TANESCO mkoa wa Singida, Maclean Mbonile akiwa ofisini kwake kutekeleza majukumu yake ya kila siku.SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa singida linatarajia kutumia zaidi ya shs. 48.3 bilioni kugharamiwa awamu mbili za miradi ya usambazaji umeme vijijini chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN). Akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibun, Meneja wa TANESCO mkoa wa singida, Maclean Mbonile amesema miradi yote inafadhiliwa na wakala wa nishati vijijini (REA ). Amesema awamu ya kwanza utekelezaji wake ilianza julai 2010 na kukamilika mwishoni mwa Septemba mwaka jana. Awamu hiyo imegharimu...

Bil. 1.5/- kutumika kubadili maisha ya Wahadzabe

Baadhi ya wanajamii ya Wahadzabe inayoishi Wilayan Mkalama mkoani Singida.   Zaidi  ya Sh. bilioni 1.5 zitatumika kusaidia jamii ya Wahadzabe inayoishi Wilayan Mkalama mkoani Singida ili ibadili maisha yao kutoka kutegemea mizizi, nyama na matunda pori kama chakula chao kikuu hadi kuwa watu wanaojishughulisha na maisha ya kisasa.  Fedha hizo amabazo zitatokana na vyanzo mbalimbali ikiwamo serikali, wafadhili na wahisani, zitatumika kuhifadhi msitu wao wa asili, kuweka miundombinu ya maji, elimu, barabara, kilimo na ufugaji bora kulingana na mahitaji ya matumizi bora ya ardhi yao. Kwa mujibu wa Ofisa Maendeleo...

Wauguzi Kilimatinde walia ukata

Na Salesi Malula-Manyoni   Wauguzi wa Hospitai ya Kilimatinde wilayani Manyoni Mkoani Singida wako katika hali mbaya kifedha kutokana na kutolipwa mishahara yao kwa muda wa miezi mitatu ambapo hawajui hadi hivi sasa hatma yao itakuwaje. Katika mahojiano maalum na Fullshangweblog timu ya wauguzi wanaofanyakazi kazi katika Hospitari hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Anglicana Dayosisi ya Bonde la Ufa wamesema wanasikitishwa sana na uongozi wa Hospitari hiyo kutowathamini na kuwacheleweshea mishahara huku baadhi ya madaktari wakiwa wamelipwa huku wauguzi tukiwa tunalia njaa kwani miezi mitatu...

Maadhimisho kupinga ukeketaji kufanyika Singida

KUKITHIRI kwa vitendo vya ukeketaji kwa watoto wachanga katika Mkoa wa Singida, kumefanya maadhimisho ya kupinga vitendo hivyo kwa mwaka huu kufanyika mkoani humo ili kutoa elimu kwa wananchi. Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Imelda Urio,  alitoa kauli hiyo jijini Dae es Salaam jana kwa niaba ya Mtandao wa Kupinga Ukeketaji unaojumuisha jumla ya mashirika 12. Urio alisema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Februari 6, wanaamini wataweza kufikisha elimu  ya kupinga vitendo hivyo ambavyo vina athari kwa watoto na wanawake. Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, mtandao ulishajaribu kupambana na vitendo hivyo kwa kuwakagua watoto pindi wanapopelekwa kiliniki, lakini zoezi hilo lilishindikana...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa