Kisima chagharimu Sh22 milioni

Gasper Andrew, Singida  MBUNGE wa Jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji, ametumia zaidi ya Sh 22 milioni, kugharamia uchimbaji wa kisima kirefu cha maji cha kitongoji cha Mtisi, kata ya Mtamaa.   Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kisima alisema, fedha hizo zimetumika pamoja na mambo mengine,kufanyia  utafiti wa eneo lenye maji,uchimbaji  na ununuzi wa pampu ya mkono.   “Hapa naomba niweke mambo wazi, gharama hii inajumuisha pia uchimbaji wa kisima ambacho kwa bahati mbaya baada ya uchimbaji kina kirefu sana, kikawa hakina maji.  Pamoja na kukosekana huko kwa maji, lakini fedha nyingi  ilitumika”,alifafanua.   Dewji alisema, ameamua kutumia fedha zake binafsi kugharamia uchimbaji huo wa kisima, kwa lengo la...

‘Acheni kuvamia migodi yenye leseni’

Gasper Andrew, Shelui OFISI ya madini Kanda ya Kati imewataka wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi wa Sekenke Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, kuacha tabia ya kuvamia maeneo yenye leseni na kuanza kuendesha shughuli zao kinyume cha sheria. Tamko hilo la ofisi ya madini, limekuja kufuatia mgogoro uliotokana na wachimbaji wadogo kugoma kuondoka wala kuingia ubia na mwenye leseni katika eneo hilo kwa madai kuwa wapo kwa muda mrefu na leseni husika kutaja Kijiji cha Mgongo badala ya Sekenke. Akizungumza mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iramba juzi, Kamishna msaidizi wa madini Kanda ya Kati, Manase Mbasha alisema kitendo cha wachimbaji hao kuvamia eneo lenye leseni na kugoma kuondoka kinakiuka sheria ya madini namba sita ya mwaka 2010 na walipaswa kushtakiwa. Kutokana...

RC apiga marufuku walanguzi wa alizeti

na Hillary Shoo, SingidaMKUU wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amepiga marufuku wanunuzi binafsi wa alizeti kununua moja kwa moja zao hilo kutoka kwa wakulima kuanzia sasa.Badala yake amewataka wakulima kuuza mazao yao kwenye vyama vya ushirika vya msingi kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ili kunufaika na zao hilo.Aliyasema hayo jana ofisini kwake alipokuwa akizungumza na viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi 81 vya mkoani hapa.“Kuanzia leo na kuendelea vyama vya ushirika vya msingi ndiyo pekee vitaruhusiwa kununua zao la alizeti kutoka kwa wakulima na wanunuzi binafsi watanunua kwenye maghala kwa maelekezo ya chama kikuu cha ushirika (SIFACU) na kwa bei watakayokubaliana.” Alisisitiza Kone.Kone alisema wanunuzi binafsi wamekuwa wakinunua zao hilo kwa wakulima kwa bei ndogo kwa...

Atalikiwa kwa kuzaa ‘nyani’

na Jumbe Ismailly, SingidaMWANAMKE mmoja, Mwanaharusi Juma (34) mkazi wa Kijiji cha Ndulungu Wilaya ya Iramba mkoani hapa, amekimbiwa na mumewe kutokana na kujifungua watoto wawili wanaofanana na nyani.Mama huyo mwenye familia ya watoto wanne wenye baba wawili tofauti, aliolewa na mume wa kwanza na kuzaa naye mtoto mmoja, Fadhila Juma (15) mwaka 2007 - mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ndulungu, kabla ya kuolewa na Sadick Selemani ambaye amemkimbia baada ya kumzalia watoto hao wawili wenye kasoro kimaumbile.“Niliolewa na Sadick mwaka 2008 na nimeishi naye kwa miaka kumi nikampatia watoto watatu, wakiwemo wawili wanaofanana na nyani, na mmoja alikuwa kawaida kama binadamu wengine,” alisema.Alisema kuwa watoto hao licha ya kuwa binadamu, lakini wamekuwa na sura za wanyama.Mama...

Dewji kutoa mamilioni kusaidia kilimo

Mwandishi Wetu, SingidaMBUNGE wa Jimbo la Singida mjini (CCM),  Mohamed  Dewji, ameahidi kuwapa wananchi wa jimbo lake Sh250 milioni, lengo likiwa ni kugharamia mradi wa kilimo katika eneo hilo. Akizungumza jimboni kwake katika hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji cha kitongoji cha Mtisi, Kijiji cha Mtamaa alisema,  fedha hizo zitatumika kununua tani 60 za mbegu za choroko, dengu na mbaazi katika msimu ujao wa kilimo. Dewji alisema  lengo la mradi huo  ni kuwajengea mazingira mazuri wakulima wa jimbo lake ili waweze   kuboresha hali zao  kiuchumi. Alisema pia kuwa, kila kikundu cha wakulima 25, kitapewa jembe la kukokotwa na wanyama (plau).“Mimi, madiwani pamoja na watendaji, tutawahamasisha wakulima kila kaya ilime ekari moja ya mazao hayo ya mbaazi, dengu...

MKAZI WA SINGIDA JELA MIAKA 30 BAADA YA KUKIRI KULAWITI MVULANA WA MIAKA 9.

Bango la mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.Picha  na Nathaniel Limu.Na Nathaniel Limu.Kijana mkulima wa kijiji cha Ihanja jimbo la Singida Magharibi Samwel Simon (22) amehukumiwa kutumikia jela miaka 30 baada ya kukiri kosa la kumlawiti kijana wa kiume mwenye umri wa miaka tisa (jina tunalo).Mvulana huyo mdogo ni mkazi wa kijiji cha Nkhoiree tarafa ya Ihanja jimbo la Singida Magharibi.Awali mwendesha mashitaka inspekta msaidizi wa polisi Shukurani Magafu, alidai mbele ya hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida Terrysophia Tesha kuwa mnamo juni 12 mwaka huu katika muda ambao haujafahamika, mshitakiwa Samwel alimlawiti mvulana...

Mtoto Wa Afrika Ilivyokuwa Singida

Watoto wa Kompasheni, Kanisa la Moravian Singida Mjini wakifuatilia moja ya tukio, maadhimisho ya mtoto wa Afrika,Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tumaini, Mjini Singida iliyo maalumu kwa wasiosikia, wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmiMkurugenzi wa Manispaa Singida, Mathias Mwangu(katikati), Afisa maendeleo jamii, Daffi Imanuel(kushoto), na mmoja wa ofisa kati Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tumaini, Mjini Singida iliyo maalumu kwa wasiosikia, wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Na Elisante John, Singida Juni 17, 2012:ZAIDI ya watoto 2,900 wanaishi mazingira hatarishi Manispaa ya Singida, hivyo kuchochea vitendo viovu,...

MBUNGE WA SINGIDA MJINI(CCM)MOHAMMED DEWJI AWAKABIDHI PIKIPIKI ZENYE THAMANI YA MILION 20 WAFANYA BIASHARA YA BODABODA SINGIDA.

 Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akizungumza na wafanyabiashara wa bodaboda (hawapo kwenye picha) muda mfupi kabla hajawakabidhi msaada wa pikipiki kumi zenye thamani ya shilingi milioni 20.Kushoto ni katibu wa umoja wa wafanyabiashara wa bodaboda, Maulid Mpondo.Kulia wa kwanza ni Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida,Williamu Haaly na anayefuata,ni katibu wa CCM manispaa ya Singida.   Mo akizungumza na waumini wa kanisa la Pentekosti la kijiji cha Ititi muda mfupi kabla hajakabidhi msaada wa mifuko 25 ya saruji na shilingi laki tano taslimu. Mmoja wa wafanyabiashara wa bodaboda akisoma...

Wakulima washauriwa kuunda mtandao kukabiliana na athari za ukame

Nathaniel Limu, SingidaWataalam wa kilimo kwenye maeneo ambayo ukame umekithiri hapa nchini, wameshauriwa kuunda mtandao wa mawasiliano, utakaosaidia kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na athari zinazosababishwa na ukame.Changamoto hiyo imetolewa juzi na katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan wakati akifungua semina ya siku tatu iliyohusu  kilimo bora cha mtama iliyohuduriwa na wataalamu 47 kutoka wilaya nane za hapa nchini.Alisema hivi sasa ukame unaosababishwa na uhaba wa mvua, unasababisha pamoja na mambo mengine, uhaba mkubwa wa mavuno ya mazoa ya chakula.Akifafanua, Liana alisema uhaba huo wa mavuno ya chakula unasababisha baadhi ya maeneo kuwa na njaa kali na hivyo wakazi wake, kushindwa kujiletea maendeleo endelevu.Aidha, Katibu tawala huyo, amewataka wananchi waishio...

Askari Magereza aua fundi kwa risasi

Na Jumbe Ismailly, Singida MKAZI wa mjini Singida, Muna Abubakari (37) ambaye ni fundi ujenzi, amefariki dunia juzi baada ya kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Magereza mkoani hapa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa saba mchana.Alisema askari aliyehusika na tukio hilo ametambuliwa kwa jina la CPL Abdalla Kabwe (31) na kwamba baada ya kutekeleza azma yake hiyo alitoroka na haijulikana alikokwenda.Alisema kabla ya tukio hilo, Abubakar alikuwa na askari wa gereza huyo wakijenga katika jengo la ofisi mpya ya jeshi hilo iliyopo maeneo ya Mtaa wa Bomani.Alieleza kuwa wakati wakiendelea na ujenzi huo ndipo askari wa kawaida wa magereza aliyetambulika kwa jina la Fred John (24) alimkabidhi bosi wake, CPL Kabwe bunduki aina...

MBUNGE WA IRAMBA MAGHARIBI MH. MWIGULLU LAMECK KUWASILISHA HOJA BINAFSI.

Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi na katibu wa uchumi na fedha CCM taifa Mwigullu Lameck Nchemba,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kusudio  lake la kuwasilisha hoja binafsi ya kuundwa kwa baraza maalum la kushughulikia makosa ya uhujumu uchumi na rushwa.Picha na Nathaniel Limu. MBUNGE wa jimbo la Iramba magharibi (CCM) mkoani Singida, Mwigulu Nchemba, anakusudia kuwasilisha hoja binafsi wakati wa bunge la bajeti lijalo, juu ya kuanzishwa kwa baraza maalum litakaloshughulikia makosa ya uhujumu uchumi na vitendo vya rushwa. Amesema amefikia uamuzi huo ambao amedai utasadia kwa kiasi kikubwa wananchi kuendelea...

HALMASHAURI YA SINGIDA KUWEKA TARATIBU NA SHERIA ZITAKAZOHIMIZA WANANCHI KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO.

   Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone,akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC),  Kulia ni katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan. Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Singida walioshiriki Kikao kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini singida.Picha zote na Nathaniel Limu.IMEELEZWA kwamba halmashauri ya wilaya ya Singida,imeshindwa kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa mapato ya ndani,kwa kile kilichodaiwa kuwa wananchi wa jimbo la Singida mashariki,kuzuiwa kuchangia maendeleo yao.Hayo yamesemwa juzi na mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Illuminata Mwenda,wakati...

NAPE AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFANI SINGIDA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Singida baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja leo Juni Mosi, 2012. Katibu tawala wa mkoa wa Singida, Liana Hassan (wapili kulia) akionyesha ramani ya jengo la utawala la hospitali ya rufani ya Singida ambayo ujenzi unaendelea. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida, Jerome Alute Nape akikagua ndani ya majengo ya hospitani ya rufani Singida Ofisa Tawala wa mkoa wa Singida, Liana Hassan (kushoto) akimpa maelezo Nape kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo ulipofika. Kulia ni AluteNape na ujumbe wake wakikagua jengo la Wazazi la hospitali ya Rufani...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa