Wananchi wa mji wa Singida wakiwa wamekusanyika nje ya viwanja vya chumba cha kuhifadhia maiti ktk hospitali ya mkoa wa Singida
Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Singida wakijiandaa kumsaidia mmoja wa majeruhi wa ajali ya lori iliyotokea wakati wakienda mna
Na: Elisante John-Singida
WATU wanane wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea mjini Singida kwa kuhusisha magari mawili, ikiwemo Landrover ya polisi na kusababisha jumla ya majeruhi 25. Ajali hizo zimetokea jana (14/9/2012) moja saa 5:30 asubuhi na nyingine saa 6:30 mchana.
Landrover ya polisi iliyohusika na ajali hiyo ni namba PT 1149 kutoka mkoni Morogoro ikiwa na abiria 11 waliokuwa wanasindikiza mwili wa askari polisi Regu Kamamo, kwenda Musoma kwa ajili ya maziko.
Kamanda wa polisi mkoa mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa alisema kuwa gari hilo lilipata ajali katika kambi ya Wachina iliyopo eneo la Manguajunki nje kidogo ya mji wa Singida.Aliwataja walifariki katika ajali iliyohusisha gari la polisi ni, staff sajenti Rose Mary Nyaruzoki (53), Nyamwenda Juma, Rehema Juma.
Sinzuma alisema uchunguzi zaidi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo huku akifafanua kuwa majeruhi wanane wa ajali hiyo wamelazwa hospitali ya mkoa Singida na hali zao zinaendelea vizuri.
Katika tukio la pili, alisema lori Fusso T.126 AEU likiwa na wafanyabishara wa mnadani likitokea Singida mjini kwenda mnada wa Mtavira kata ya Minyunge wilaya ya Singida, lilipinduka na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 17
Alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 6.30 mchana katika kijiji cha Mtavira, Singida vijijini.Aliwataja waliofariki dunia papo hapo ni Sarafina Ally, Pili Saida, Charles Thomas na wengine wawili waliofahamika kwa jina moja moja la Bakari na Bilali.
Alisema chanzo cha ajili ya fuso,bado hakijafahamika na uchunguzi zaidi bado unaendelea. Hata hivyo Sinzumwa alisema taarifa kamili kuhusiana na ajali hizo, atazitoa kesho (leo 15/9/2012) .Mganga mfawidhi hospitali ya mkoa Singida, Dk. Joseph Malunde alisema majeruhi hao 17, wamelazwa hospitali ya mkoa wa Singida na hali zao zinaendelea vizuri.
"Maiti zote tisa pamoja na ile ya askari aliyekuwa anasafirishwa na gari la polisi na zile za Fusso, zimehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa,"alisema Dk. Malunde.
Kwa mjubu wa mmoja wa majeruhi wa fuso,Maulidi Mohammed,fuso hilo lilipinduka baada ya breki zake kufeli likiwa kwenye mteremko mkali hali iliyosababisha dereva ambaye hata hivyo hajafahamika ashindwe kulimudu.
0 comments:
Post a Comment