Home » » TUNDU LISSU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

TUNDU LISSU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

Baba mzazi wa mheshimiwa Tundu Antipas Lissu Mughwai na Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita. Marehemu Augostino Lissu Mughwai (84) amefariki katika hospitali ya taifa ya muhimbili alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu. Mungu amlaze mahala pema peponi, Amina. Chadema Blog inapenda kuchukua nafasi hii kukupa pole Mh Tundu Lissu kwa kufiwa na Baba Mzazi. Tupo pamoja nawe katika kipindi hiki cha Majonzi na Mwenyezi Mungu amlaze mzee wetu Mahali pema Peponi, Amina.SOURCE CHADEMA

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa