Na.Nathaniel Limu-Singida.
Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi unaohusisha wanafunzi 27,749 wa darasa la saba mkoani Singida umeanza kwa amani na utulivu licha ya kujitokeza kwa kasoro ndogondogo.
Miongoni mwa kasoro hizo ni pamoja na utoro, baadhi ya wanafunzi kutojua kusoma na kuandika na walimu na wasimamizi kulalamikia mfumo wa maswali ya kuchagua na kuweka vivuli.
Katika shule ya msingi Mtisi iliyopo umbali wa zaidi ya kilomita 24 kusini magharibi mwa mji wa Singida, wasimamizi wa mtihani huo wamesema kati ya 34 watahiniwa nane (8) hawakufanya mtihani kutokana na utoro na wengine sita wameshindwa kusoma wala kuandika.
Hata hivyo afisa elimu mkoa wa Singida Yusuf Kipengele, amesema mbali ya kasoro hizo hakuna dosari nyingine kubwa iliyojitokeza na kuathiri ufanyaji huo wa mtihani ulioanza leo.
Kipengele ametoa wito kwa wasimamizi wa mtihani huo kuwa waadilifu na kutojihusisha na udanganyifu vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria pindi watakapobainika.
0 comments:
Post a Comment