Home » » MACHAFUKO MWENYEKITI UWT MKALAMA

MACHAFUKO MWENYEKITI UWT MKALAMA

na Jumbe Ismailly, Iramba
MKUTANO Mkuu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) ya CCM Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, umemchagua Elipendo James Machafuko kuwa mwenyekiti wa jumuiya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Machafuko alinyakua nafasi hiyo baada ya kupata kura 239 kati ya 399 zilizopigwa na kuwashinda wagombea wengine; Mariamu Hussein Kahola aliyepata kura 115 na Magreth Hussein Kinota aliyepata kura 35.
Akitangaza matokeo, msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Fatma Taufiq, alisema kati ya kura 399 zilizopigwa, nne ziliharibika na kura halali zilikuwa 389.
Kwa mujibu wa Taufiq ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Manyoni, wajumbe watatu walioshinda nafasi ya Mkutano Mkuu Taifa na kura zao zikiwa kwenye mabano ni Helena Msengi Kitila (253), Habiba Issa Kununta (240) na Sara Aroni Mwambu (161).
Wajumbe wengine waliogombea nafasi hiyo na kura zao kutotosha ni Sara Samson Mlinga (kura 145), Mariamu Hussein Kahola (112), Christina Ng’aida (86), Hadija Said Magolanga (64) na Hawa Mawele (60). Kura zilizopigwa ni 393, zilizoharibika ni 14 na kura halali ni 376.
Aidha, Taufiq alisema Hadija Saidi Magolanga (kura 203), Sara Aron Mwamba (198) na Fatuma Shillah (169) wamechaguliwa kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2011. Singida Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogz za Mikoa