Mwandishi wetu, Singida Yetu
KIKOSI cha askari wa usalama barabarani mkoani Singida kimekusanya zaidi ya shilingi milioni 53.1 kutokana na faini mbalimbali zilizotozwa kwa wadau wa usafiri na usafirishaji kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Kamanda jeshi la polisi mkoani humo Kamishina msaidizi Linus Sinzumwa amesema fedha hizo zimetokana na makosa 1842 ya kukiukwa kwa sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani.
Kamanda Sinzumwa ameyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni pamoja na mwendo kasi kwa madereva, kutofunga mkanda, ulevi wakati wa kuendesha gari, kutokuwa na kibali cha barabarani, magari mabovu na kutozingatia alama za usalama barabarani.
Ametoa wito kwa wadau wote sekta ya usafiri na usafirishaji kujenga uatamaduni wa kuzingatia sheria zote muhimu ili kupunguza ajali hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
Hivi sasa jeshi la polisi mkoani singida lipo kwenye mchakato wa ukaguzi wa vyombo vyote vya moto ikiwa ni moja ya hatua muhimu katika kuadhimisha wiki hiyo
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment