Mkuu  wa mkoa wa Singida Dkt.Parseko Kone (mwenye suti ya bluu) akisalimiana  na mzee wa Kihadzabe mkazi wa kijiji cha Munguli kitongoji cha Kipamba  ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Mkuu  wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akihamasisha jamii ya Kihadzabe wa  kitongoji cha Kipamba kushiriki sensa ya taifa inayotarajiwa kufanyika  nchini kote Agosti 26 mwaka huu.
Mkuu  wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone (mwenye suti ya bluu)akimkabidhi  msaada wa chakula Mwenyekiti wa kitongoji cha Kipamba kijiji cha Munguli  Edward Mashimba (mwenye shati jeupe).
Maboksi  ya msaada wa chakula kilichotolewa na shirika lisilo la kiserikali la  International Outreach International na nchini Marekani. Chakula hicho  kina uzito wa zaidi ya tani moja.
Mkuu  wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone, akiwa amempakata mtoto wa  Kihadzabe aliyebatizwa jina lake la Kone. Mtoto huyo alizaliwa asubuhi  ya siku Dkt. Kone alipofanya ziara ya kwanza ya kikazi katika kijiji  hicho miaka sita iliyopita. Nyuma ya mtoto huy ni Mkuu wa wilaya ya  Singida Mwalimu Queen Mlozi.
Baadhi  ya akina mama wa Kihadazbe waliohudhuria mkutano wa hadhara ambao mkuu  wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone, aliutumia kuhamasisha jamii ya  Kihadzabe na nyingine kushiriki sensa inayaotarajiwa kufanyika Agosti 26  mwaka huu. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu.
Serikali  ya wilaya mpya  ya Mkalama mkoani SIngida imeahidi kutoa nyama pori ya  kutosha kwa Wahadzabe wa kitongoji cha Kipamba kata ya Mwangeza, ili  waweze kushiriki sensa ya kitaifa ya watu na makazi inayotarajiwa  kufanyika nchini kote Agosti 26 mwaka huu.
Kwa  mujibu wa mkuu wa wilaya hiyo Edward Ole Lenga, msaada wa nyama ya  wanyama pori hiyo, utasaidia jamii ya Wahdzabe kubaki kwenye kaya zao  kipindi chote cha sensa.
Akizungumza  muda mfupi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko  Kone, awahamasishe Wahadzabe na wakazi wengine wa kata ya Munguli,  kushiriki sensa.
Lenga  amesema msaada huo wa  nyama pori, unatokana na ombi liliotolewa na  jamii hiyo ambayo chakula chake kikuu ni nyamapori, mizizi, matunda pori  na asali.
Akifafanua  amesema Wahdzabe hao wanaokadiriwa kufikia 227, wametoa ombi hilo ili  wakati wote wa sensa wasiende porini kuwinda na badala yake wabaki  kwenye kaya zao wakisubiri kuhesabiwa.
Mkuu  huyo wa wilaya amesema ombi hilo tayari limeshakubaliwa na maandalizi  yote muhimu ya kuwinda wanyama pori siku moja kabla ya siku ya sensa,  yamekwisha kamilika.
Kwa  upande wake mkuu wa mkoa Dkt. Kone, ametoa msaada wa chakula chenye  uzito wa zaidi ya tani moja, ambacho kitakidhi mahitaji kuanzia sasa  hadi zoezi la sensa litakapokamilika.
Amesema  kwa hali hiyo, kipindi chote cha sensa, hapatakuwepo na haja kwenda  porini kutafuta wanyama pori, asali, matunda pori au mizizi.
Katika  hatua nyingine, amewataka wahakikishe kila mmoja anahesabiwa mara moja  tu, kwa madai kuwa wakishafahamika idadi yao na hali zao za maisha,  itasaidia serikali kujipanga namna bora  ya kuwahudumia na kuwaletea  maendeleo.
Wakati  huo huo Dk. Kone, amesema pamoja na kunid la wawindaji, pia makundi  mengine ya wavuvi, wachungaji wanaohama hama, watafutaji madini na  baadhi ya wakulima ambao wana mashamba yaliyo mbali na makazi au makambi  yao ya kawaida, warejee kwenye kaya na makambi yao ili waweze  kuhesabiwa siku ya sensa. 
0 comments:
Post a Comment