Kamanda wa Polisi Mkoani Singida,SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
WATU
watatu mkoani Singida wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo
la mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mng’imba Wilaya ya
Mkalama kusombwa na maji ya mto wa Ndurumo.
Kwa
Mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Singida,SACP Geofrey
Kamwela mwanafunzi huyo ni Mwajuma Jumanne mwenye umri wa miaka tisa.
Amesema
mwanafunzi huyo amesombwa na maji ya mto wa Ndurumo januari 28 mwaka
huu saa sita mchana wakati akivuka mto wa Ndurumo akitokea shuleni
akielekea nyumbani kwao.
“Mwili
wa mwanafunzi huyo ulionekana...
PSPF YAZINDUA MPANGO MPYA WA UUZAJI NYUMBA KWA BEI NAFUU, SOMA HAPA KUJUA BEI ZAKE

Mfuko
wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa
uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es
Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga
(Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).
Bei
za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei
hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo. Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili
hadi vinne.
Chini
ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji
atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na...
Shirika lisilo la kiserikali toka Uingereza lakabidhi vifaa vya thamani Tsh 20m kwa mafundi wadogo
Katibu
tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana, akizungumza kwenye hafla ya
kukabidhi vifaa kwa mafundi wadogo wa useremala,ushonaji wa nguo,uhunzi
na ujenzi.Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 20
milioni,vimetolewa na shirika la Tools for self reliance la nchini Wales
Uingereza na zimepitia SIDO mkoa wa Singida.
Katibu
tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana (wa pili kulia) akikabidhi
cherehani kwa mmoja wa kiongozi wa vikundi 17 vilivyonufaika na msaada
wa vifaa vya ufundi vilivyotolewa na shirika la Tools for self reliance
la nchini Wales Uingereza.Wa kwanza kulia ni meneja wa SIDO mkoa wa
Singida, Shoma...
Wakazi wa kanda ya kati waomba kutoa taarifa sahihi ya nguvu kazi ya Taifa
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi, akizungumza kwenye ufunguzi wa
mafunzo ya wiki mbili ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye
uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Singida ,Dodoma, Tabora na
Kigoma.Mafunzo hayo yanafanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini
Singida.
Baadhi
ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi
katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma wakiwa kwenye mafunzo
ya wiki mbili yanayohusu utafiti huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi
ujao.
Mkuu
wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya
pamoja na wadadisi na wahariri...
RC Singida ahimiza ushirikiano
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone, amewataka
wakazi wa Kanda ya Kati kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na wahariri wa
utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi, ili Serikali iweze
kutambua hali halisi ya ajira nchini. Dk Kone alitoa wito huo juzi
wakati akifungua mafunzo ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu
wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014. Alisema utafiti huo ambao
mahojiano yake yanatarajiwa kufanywa katika kaya 11,520 nchini,
unatarajiwa kuanza Februari mwaka huu na kwamba utatoa viashiria muhimu
ikiwemo kujua hali ya ajira nchini.
Chanzo;Mwananchi...
Mvua ya mawe yaharibu ekari 800 za mazao mbalimbali Ikungi.

Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Hassan Tati akikagua mashamba
ya mazao mbali mbali yaliyoharibiwa na mvua kubwa ya mawe na upepo mkali
iliyonyesha juzi katika kijiji cha Siuyu.Jumla la ekari zai ya 800
zilimeharibiwa na mvua hiyo.
ZAIDI
ya ekari 800 za mazao mbalimbali yaliyolimwa katika vitongoji vinne vya
kijiji cha Siuyu tarafa ya Mungaa wilaya ya Ikungi,zimeharibiwa vibaya
na mvua kubwa ya mawe na iliyoambatana na upepo mkali.Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Unyankhanya
wilaya ya Ikungi,Adriano Herman wakati akitoa taarifa ya uharibifu
mkubwa wa mazao kwa Mwenyekiti...
Watu wasiofahamika wamnyang’anya bunduki Mzee wa miaka 71.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.
WATU
wasiofahamika idadi na makazi yao,wamevamia nyumba ya Daudi Karata (71)
mkulima na mkazi wa kijiji cha Nguamghanga tarafa ya Mgori wilaya ya
Singida mkoa wa Singida,na kunyang’anya bunduki aina ya shot gun na
risasi zake nne.
Kabla
na kufanya unyang’anyi huo,kundi hilo la watu wasiofahamika,lilimkata
kata mapanga mzee Karata sehemu mbalimbali za mwili kwa lengo la
kufanikisha azma yao kwa urahisi zaidi.
Kamanda
wa Polisi, mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo
limetokea januari...
SIDO Singida yawataka wajasiriamali kutumia mikopo kuimarisha ndoa zao
Meneja
wa SIDO mkoa wa Singida, Shoma Kibende akitoa nasaha zake muda mfupi
kabla hajatoa mikopo yenye thamani ya shilingi 18.9 kwa wajasiriamali wa
kikundi cha Urafiki cha mjini Singida.Kulia (aliyekaa) ni katibu wa
kikundi cha urafiki,Remiji Alex.
Meneja wa SIDO mkoa wa Singida,Shoma Kibenda,akimkabidhi Remji Alex mkopo wa shilingi 500,000.
Meneja
mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Ruben Mwanja akitoa mafunzo kwa
wajasiriamali muda mfupi kabla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya
zaidi ya shilingi 18.9 milioni kwa kikundi cha urafiki cha mjini
Singida.
Meneja
mikopo wa SIDO mkoa wa Singida, Ruben Mwanja (wa kwanza...
PSPF YATOA PONGEZI KWA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA WIZARA YA FEDHA
MFUKO WA PENSHENI WA (PSPF)
SALAMU ZA PONGEZI
Waziri wa Fedha Mhe.
Saada Mkuya Salum (MB)
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Adam K. Malima.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa
kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa
Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima.
Bodi ya Wadhamini...
JUSTIN: WATU WANAODADIKIKA KUFIKIA 13 WAMEFARIKI KATIKA AJALI SINGIDA.
Imetokea ajali mbaya huko Singida ambapo gari aina ya NOAH na Lori la mizigo yamegongana uso kwa uso na kisha gari hiyo aina ya NOAH kuingia chini ya uvungu wa Lori na kusababisha vifo vya watu hao 13 ambao wote walifia katika eneo la ajali.Taarifa inasema gari aina ya NOAH ilikuwa imebeba abiria kutoka Itigi wakielekea Singida Mjini.Dereva na utingo wa Lori walikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.CHANZO: ITV breaking News....
Msindai: Lowassa jembe la maendeleo
Aeleza anaunga mkono harakati zake za maendeleo Akanusha kuzungumzia masuala ya urais Monduli
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mikoa wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Singida,
Mgana Msindai,akiongea na waandishi wa habari jana.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mgana Msindai amekanusha vikali madai kuwa amemuunga mkono,
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika suala la kuwania urais wa
mwaka 2015.
Badala yake Msindai ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,
amesema anamuunga mkono kwa nguvu zote Lowassa katika juhudi zake...
BASI LA SHABIBY LAPATA AJALI,28 WAJERUHIWA
ABIRIA 28 wakiwemo
watoto wanne, wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Shabiby namba T
930 BUW, aina ya Utom, walilokuwa wakisafiria kugongana na lori la
mafuta na kupinduka katika Kijiji cha Kisaki. Ajali hiyo imetokea
jana mchana umbali wakilomita 10 kutoka mkoani Singida kwenda Dodoma
wakati dereva wa basi hilo akijaribu kulipita lori upande wa kulia .Lori
hilo lenye namba RAA 486N, aina ya Mercedes Benz, lilikuwa likitokea
Kigali, nchini Rwanda, kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Barimina
Benjamin (37).Inadaiwa basi hilo lilikuwa na abiria 48 ambapo dereva
wake alikimbia baada ya ajali. Baadhi ya majeruhi waliozungumza na
Majira, walisema majeruhi wa ajali hiyo ni pamoja na kondakta...
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) UNAWATAKIA WATU WOTE SIKUKUU NJEMA MAULID

JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (Swalla
Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Waisalamu na Watanzania
wote katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
alayhi wa aalihi wa sallam)
“PSPF TULIZO LA
WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu,
PS...
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) UNAWATAKIA WATU WOTE SIKUKUU NJEMA MAULID

JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (Swalla
Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi
wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Waisalamu na Watanzania
wote katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu
alayhi wa aalihi wa sallam)
“PSPF TULIZO LA
WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu,
PS...
DIWANI; WATENDAJI WANAOKULA FEDHA WACHAPWE VIBOKO
DIWANI wa Rungwa, Tarafa ya Itigi, wilayani Manyoni, Singida,
Edward Machapaa, amependekeza adhabu ya kuchapwa viboko itolewe kwa
watendaji wanaokula fedha za wananchi zilizotolewa na serikali kwa
ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Machapaa alitoa pendekezo hilo kwenye mkutano maalumu wa Baraza la
Madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo uliofanyika mjini Manyoni
alipokuwa akijadili hoja ya matumizi mabaya ya fedha za miradi ya
maendeleo.
Alisema kumekuwepo malalamiko mengi na ya mara kwa mara juu ya fedha
za miradi kutumika vibaya au hata kwa baadhi ya watendaji kula fedha
hizo, hivyo umefika wakati wa kubadili mbinu ya kutoa adhabu kwa kutoa
adhabu ya viboko.
“Ndugu mkurugenzi, kwa...
SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO
WA PENSHENI WA PSPF
Bodi
ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
wanaungana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheni pamoja
na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya
Zanzibar, 12 Januari 2014.
Kwa
Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa
“PSPF
TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu,
PS...
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
AMIN...
HABARI MPASUKO; BASI LA ABIRIA LA MTEI LACHOMWA MOTO BAADA YA KUGONGA BODABODA NA KUUA WATU (3)

Leo asubuhi basi la abiria la kampuni ya Mtei toka Arusha limechomwa moto na wananchi wenye hasira maeneo ya Njia panda Mnadani, mkoani Singida baada ya bus hilo kugonga pikipiki yaani bodaboda na kuua watu watatu hapo hapo. Zifuatazo ni taswira za basi hilo lililokuwa wakati na baada ya kuchomwa moto
Chanzo michuzi blog
...
MBEGU NA PEMBEJEO BORA VYACHANGIA ONGEZEKO LA UZALISHAJI WA ALZETI SINGIDA
MATUMIZI mbegu bora na
pembejeo nyingine za kilimo pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalamu,
vimetajwa kusaidia kuongeza mara dufu kiwango cha uzalishaji wa zao la alzeti
mkoani Singida.
Mtaalamu wa kilimo cha zao hilo
kutoka halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida bwana Elias Ziwa
amebainisha hayo katika taarifa yake juu ya mafanikio na changamoto
za kilimo cha Alizeti
Amesema kuwa uzalishaji alzeti
ambayo ndio zao kuu la biashara kwa wakazi wa mkoa huo, umeongezeka
kutoka magunia 4 kwa ekari miaka mitano iliyopita, hadi kufikia zaidi ya
gunia 12 hivi sasa.
Hata hivyo amesema pamoja na ongezeko hilo
amesema wameweka mkakati wa kuendelea kutoa elimu zaidi ili kufikia
hatua ya baadhi ya wakulima...
WADAU WA AFYA SINGIDA WARIDHIA MFUMO WA TIBA KWA KADI
Mkuu
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone akizungumza kwenye uzinduzi
wa mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika halmshauri ya manispaa ya
Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae Resort mjini
Singida. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi.
Meneja
msaidizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Singida, Isaya
Shekifu, akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa
Singida.Dk.Parseko Kone, kuzindua mfuko wa Tiba kwa kadi (TIKA) katika
manispaa ya Singida. Walioketi kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya
Iramba,Yahaya Nawanda na Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh
Salumu Mahami.
Mkuu
...